Natumai mu wazima wa afya.
Naombeni msaada wenu tafadhali ni sababu zipi husababisha kiuno kuuma mara kwa mara hasa nyakati za jioni kwa mjamzito wa wiki kama saba hivi.
Tatizo hili limedumu kwa muda sasa (kama wiki tatu hivi) na hospital wanasema ni hali ya kawaida itaisha tu.
Ni hali inayotia wasiwasi hasa ukizingatia ni moja ya dalili za hatari kwa mjamzito na pia mtu mwenyewe hafanyi kazi yoyote nzito na muda wote huo amekuwa akishinda nyumbani.
Kwa mwenye uelewa au uzoefu na hii hali naomba msaada tafadhali.