mimi ni mama wa mtoto mmoja (nategemea mwingine Mungu akijalia mapema mwakani),ana umri wa miaka mitatu,tatizo lake ni kuwa jamani hataki kula,nimejitahdi kadiri niwezavyo lakini sioni mafanikio.Hospitali,kumbembeleza lakini wapi sanasana ataishia kujitapisha,sasa napatwa na hasira hadi nampiga alafu baadae naanza kujuta kwa nini nilimpiga.Yani hapa nilipo nina hasira maana nimejaribu kumbadilishia vyakula lakini wapi,kama hapa sasa hivi nimeishia kumuwasha vibao akalia na kutapika juu.jamani mwenye msaada wa kunisaidia naomba afanye hivyo tafadhali.asante.