msaada tafadhali wa mawazo na kiafya kwa mwanangu.

prax

Member
Joined
Mar 13, 2013
Posts
27
Reaction score
8
mimi ni mama wa mtoto mmoja (nategemea mwingine Mungu akijalia mapema mwakani),ana umri wa miaka mitatu,tatizo lake ni kuwa jamani hataki kula,nimejitahdi kadiri niwezavyo lakini sioni mafanikio.Hospitali,kumbembeleza lakini wapi sanasana ataishia kujitapisha,sasa napatwa na hasira hadi nampiga alafu baadae naanza kujuta kwa nini nilimpiga.Yani hapa nilipo nina hasira maana nimejaribu kumbadilishia vyakula lakini wapi,kama hapa sasa hivi nimeishia kumuwasha vibao akalia na kutapika juu.jamani mwenye msaada wa kunisaidia naomba afanye hivyo tafadhali.asante.
 
Kama umeona suluhu ya tatizo la mwanao ni makofi basi endelea kumzaba vibao usiache mpaka aanze kula,.,
 
mimi ni mama wa mtoto mmoja (nategemea mwingine Mungu akijalia mapema mwakani),ana umri wa miaka mitatu,tatizo lake ni kuwa jamani hataki kula,nimejitahdi kadiri niwezavyo lakini sioni mafanikio.Hospitali,kumbembeleza lakini wapi sanasana ataishia kujitapisha,sasa napatwa na hasira hadi nampiga alafu baadae naanza kujuta kwa nini nilimpiga.Yani hapa nilipo nina hasira maana nimejaribu kumbadilishia vyakula lakini wapi,kama hapa sasa hivi nimeishia kumuwasha vibao akalia na kutapika juu.jamani mwenye msaada wa kunisaidia naomba afanye hivyo tafadhali.asante.
Sikushauri umpige mtoto kabisa dada yangu KUMBUKA HUYO NI MTOTO NA HAJUI HATA KOSA LAKE MASKINI MALAIKA WA MUNGU!!Nimesikitika sana kusikia miaka 3 anapigwa!!Au ndo homoni za ujauzito zimekuzidi?
Mtoto wa miaka mitatu anaweza kula chakula cha kawaida cha mtu mzima!Kwanini unampa vyakula laini wakati ana meno na anaweza kutafuna!

  • Mpe vyakula vya kawaida kama wali na mchuzi,muwekee mbogamboga kwenye mchuzi(vegetables),
  • Mpe matunda tofauti mkatie vipande uchanganye matunda yenye rangi tofauti na ladha tofauti ikiwezakana mtengenezee SMILEY FACE KWA matunda au mbogamboga kama kwenye picha chini ...fanya chakula kama mchezo atakula(MAKE FOOD FUN)..Watoto wanapenda michezo...
  • Lazima ww kama mzazi umpe motivation ya kula ukimpiga maanake anafanya makosa kutokula na si sahihi kwasababu inawezekana hapendi ladha ya hiko chakula anachopewa!!Isitoshe anajenga UWOGA ni kitu ambacho kinaweza kumuathiri ulaji wake!!Kwasababu atakuwa anakula kwa sababu anaogopa kupigwa hali kwasababu ana njaa au anapenda ladha ya chakula..Kutapika ni lazima kwasababu nina taswira tayari analia na unamsokomeza chakula lazima kitoke!!
  • Ni muhimu sana tufikirie matendo yetu katika ulezi wa mtoto!
View attachment 112641
View attachment 112642

Tembelea link hii kwa ujuzi zaidi kuhusu vyakula vya watoto:
CULINARY CHAMBER Tanzanian Executive Chef Issa Kapande: Search results for chakula cha watoto
 
We need people like u!! Ushauri mzuri sana !!
 
Back
Top Bottom