Msaada tafadhali, Wajuzi wa mambo, kujeni hapa.

herzegovina

JF-Expert Member
Joined
Oct 28, 2015
Posts
3,143
Reaction score
4,724
Wakuu naomba mnipe muongozo hapa.

Chombo kikuu cha kutoa haki ni mahakama. Sasa nauliza, kama mahakama ikiizuia serikali kufanya jambo fulani, au ikiiamuru serikali kulipa gharama fulani na serikali isitekeleze.....ni kipi kinatakiwa kifanyike???

Na hii siyo kwa serikali tu, hata viongoz wa serikali. Tuliona hukumu dhidi ya bwana mrisho Gambo, sidhani kama alilipa kile alichotakiwa kulipa kwa amri ya mahakama.

Hii ina maana hata kesi ya mbowe dhidi ya DC wa hai inaweza kuishia juu kwa juu....

Mimi naomba mnijuze, serikali ikikaidi amri ya mahakama ni kipi kinatakiwa kifanyike???
 
Ni kusamehe 7×70=490 Maana serikali ikiwa ya kidikteta hata wewe ulivyohoji hapa watataka wakupime mkojo

Kwa Hisani Ya Watu Wa Mbeya!
 
Unaongelea ule muhimili uliojishindilia zaidi au?
Wameshasema watailinda katiba ndio wanailinda sasa shida nini?
 
Mara chache nafikiri hilo limekuwa likitokea la Serikali kukaidi hukumu za Mahakama..

Na kiukweli wala sina reference za kesi ambazo Serikali ilikataa ku comply..

But kwa case ya Mrisho Gambo ile ni individual case.. Hata ya Mbowe amemshitaki yule DC kama individual.

Sasa kwa Gambo hajalipa ile penalty mpaka leo na mahakama ipo kimya tu.

Sijui kwanini Mahakama inakubali kudharaulika namna hii.
 
Najua Ile ni individual case....lakini kwa vyovyote vile kuna mkono wa serikali unaompa kiburi...je ni nini kinatakiwa kifanyike?
 
Najua Ile ni individual case....lakini kwa vyovyote vile kuna mkono wa serikali unaompa kiburi...je ni nini kinatakiwa kifanyike?
Nafikiri anaetakiwa kulipwa fidia lazima alalamike kwa hukumu husika kutotekelezwa Mkuu..
Then Mahakama ndio iingilie kati.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…