heshima kwenu wakuu, kuna jamaa yangu anaishi maeneo ya Tabora ana dumu zaidi ya 20 za lita ishirini kila moja za asali na anatafuta soko.anataka azitume nimuuzie but kwa hapa Dar es salaam me sijui soko la asali mbichi liko wapi.miaka ya nyuma aliwahi kutuma kama tatu hivi nikamuuzia coz kuna mtu alikuwa anataka kwa matumizi yake binafsi.now jamaa inaonekana anahitaji sana pesa ndo hivyo tena pressure inazidi.naomba msaada kama kuna mwana JF yeyote anafahamu soko au sehemu wananunua asali mbichi anijuze coz inaweza kuwa biznez ambayo ni nzuri.natanguliza shukrani.