Msaada tafadhali...!!

Msaada tafadhali...!!

OGOPASANA

JF-Expert Member
Joined
Apr 30, 2009
Posts
262
Reaction score
144
Habari wakuu, nahitaji msaada wa kupata mkopo wa kiasi cha shillingi milioni mia moja (100 Mil) kutoka kwa mtu binafsi ama taasisi yoyote kwa ajili ya kufufua, kuboresha na kuendeleza biashara zangu. Nina mdhamini (mama yangu) aliye tayari kunidhamini kwa ajili ya mkopo huu kwa kuweka dhamana nyumba mbili (moja ina vyumba vitatu, sitting room, dinning room, jiko na nyumba nyingine ina vyumba kumi mfumo wa vyumba vitano kushoto na vitano kulia). Nimejaribu kutafuta na kupata mkopo katika mabenki na taasisi nyingi za kifedha bila mafanikio kwa kuwa wanasema biashara zangu ndo zilikuwa zinaanza walau ningekuwa na uzoefu usiopungua mwaka mmoja na kuendelea. Nina uwezo wa kulipa riba isiyozidi asilimia tatu (3%) kwa mwezi au asilimia arobaini (40%) kwa mwaka. Nina uwezo wa kurejesha mkopo kuanzia mwaka mmoja hadi miaka mitatu. Kwa yoyote anayeweza kunisaidia kwa lolote kuhusiana na suala hili anisaidie tafadhali.

Mwombaji mkopo - 0654 743 825
 
Nyumba ziko wapi hizo kiongozi?[/QUOTE]

Nyumba moja ipo Majohe kwa Ngonzoma na nyingine ipo Msongola (karibu na Chanika au Mvuti)- Dar Es Salaam.
 
Jina lako sasa...

Haya ni majina tu (ID Nick names) katika kuficha uhalisia wa mtu katika mitandao hii ya kijamii, lakini haina uhusiano wa moja kwa moja na mtu jinsi alivyo. Na mara nyingi wale wenye sifa mbaya ndo hupenda kutumia majina mazuri na wenye sifa nzuri hupenda kutumia majina ya kipekee na ya ajabu.
 
Wana jf p'se hasa wa morogoro mnijuze natarajia kuhamia moro na kujiajiri yani kufungua kama mgahawa mdogo ila wa kileo,product zangu naoka mwenye we kama cake sambu sa natengeneza pure fruits juices na vingin evyo je moro kutani weka ktk hali ya mat umaini?p'se nasubiria majibu yenu.thanx
 
Mtaji 1m vifaa vingine ninavyo kama majiko fridge machine za juice na vyombo vya walaji
 
Wana jf p'se hasa wa morogoro mnijuze natarajia kuhamia moro na kujiajiri yani kufungua kama mgahawa mdogo ila wa kileo,product zangu naoka mwenye we kama cake sambu sa natengeneza pure fruits juices na vingin evyo je moro kutani weka ktk hali ya mat umaini?p'se nasubiria majibu yenu.thanx
unaharibu mtiririko wa thread ya mwenzio ,kwaa nini usifungue yako kama upo serious??? watu wengine bwana!
 
kwa nini usianze na kiasi kidogo, kopa hata kwa benki 2 tofauti hata 10M kila moja, lipa ndani ya miezi 4 kujenga uaminifu! then kopa tena 20M kila benki, ndani ya mwaka unakuwa unakopesheka tena hata bila hizo hati za nyumba yako!
 
Nyumba zako zina hati halali?

By the way, riba ya 3% ni ndogo mno. Benki nyingi zinatoza riba kuanzia 25%. Sasa ukope kwa mtu binafsi kwa riba ya 3% sidhani kama itawezekana.
 
Kama biashara zako zinahusiana na kilimo na ufugaji kwanini usiende pale TIB(Tanzania Investiment Bank) wao wana masharti nafuu na wanachukua mpaka dhamana ya mashamba yenye hati LOCAL(hati za kienyeji)...

Nadhani ukienda na hizo hati zao utapata hata hiyo million kumi unayoihitaji maana wanatoa mpaka billion moja kwa riba nafuu sana nafikiri ni kama 19.2% kwa mwaka.......
 
Nyumba zako zina hati halali?

By the way, riba ya 3% ni ndogo mno. Benki nyingi zinatoza riba kuanzia 25%. Sasa ukope kwa mtu binafsi kwa riba ya 3% sidhani kama itawezekana.

Mkuu hiyo riba ya 25% ya mabenki kama unavyosema ni ni kwa mwaka na si kwa mwezi.
 
Kama biashara zako zinahusiana na kilimo na ufugaji kwanini usiende pale TIB(Tanzania Investiment Bank) wao wana masharti nafuu na wanachukua mpaka dhamana ya mashamba yenye hati LOCAL(hati za kienyeji)...

Nadhani ukienda na hizo hati zao utapata hata hiyo million kumi unayoihitaji maana wanatoa mpaka billion moja kwa riba nafuu sana nafikiri ni kama 19.2% kwa mwaka.......

Asante ila biashara zangu hazihusiani na kilimo wala ufugaji.
 
Hii capital injection unataka Kwa matumizi gani? Jee forecast Zako za revenue zikoje? Do you have any sales? If yes how much?
 
kwa nini usianze na kiasi kidogo, kopa hata kwa benki 2 tofauti hata 10M kila moja, lipa ndani ya miezi 4 kujenga uaminifu! then kopa tena 20M kila benki, ndani ya mwaka unakuwa unakopesheka tena hata bila hizo hati za nyumba yako!

Asante kwa ushauri mzuri mkuu, tatizo kiasi cha bajeti kinachohitajika ni Milioni 100 sasa nikichukua milioni 10 afu nirudishe kwa miezi minne itakuwa ngumu. Pia mabenki na taasisi nyingi za mikopo hawatoi mikopo kwa biashara zinazoanza (start-up) kwani nilishajaribu huko hadi nikachoka na kuona pengine labda wanatoa kwa kujuana au rushwa.
 
Back
Top Bottom