msaada tafadhali

msaada tafadhali

lufuo

Member
Joined
Feb 21, 2015
Posts
97
Reaction score
34
Nasikia nabanwa na kitu kama vichomi tumboni kwa chini hasa upande wa nyonga /diaphram baadhi ya watu wameniambia ni baridi ninywe maji au chai ya moto nimefanya hivyo lkn bado hii mi siku ya pili. Msaada kwa anaejua tatizo hili
 
we ni me au ke? kichomi kwa mda gani? nyonga upande gani? umri je?
fafanua vizuri mkuu.
Au nenda tu hospital ukapime
 
Pole sababu zipo nyingi.lakini nenda ukapime. usikwepe usipo ziba ufa utajenga ukuta.
 
Pole sana..Hospital kuna suruhisho la uhakika kama hapa hawatakuja wataalam japo Mungu ndiyo uhakika zaidi
 
Upande wa kushoto kwa chini karibu na nyonga
 
Upande wa kushoto kwa chini karibu na nyonga

Maumivu ya kichomi au kama
kichomi chini ya kitovu na
maumivu haya uwa hayawi kwa
marefu hapana yanakua sehemu
moja tu na yanakua kama
kichomi. Na maumivu haya
yanaweza kuwa ya upande mmoja
ua pande zote mbili na mara
nyingi hutokea pale mtu anapokua
akicheka au kuinama au ukiwa
unakimbia au umeinua kitu kizito,
iyo inakuonyesha kuwa wewe una
ovarian cysts. (uvimbe kwenye ovary). juchunguze uone kama yanaendana.
 
Upande wa kushoto kwa chini karibu na nyonga

kama kinakubana ukiwa unafanya mazoezi au uko bizebize, ukiwa umejipumzisha au umelala basi uchunguzwe moyo na mfumo wa damu.
 
Upande wa kushoto kwa chini karibu na nyonga

kama kinakubana ikiwa unakula, umeshiba sana au unanjaa basi ni asidi tumboni, pima ujue ni asidi gani usije ukazua vidonda vya tumbo.
 
NYONGEZA;
epuka au punguza matumizi ya;
>vinywaji baridi sana
>viungo vingi kwenye chakula hasa pilipili na binzari.
>vyakula vya mafuta.
pia usipigwe na baridi sana, vaa koti.
kama ni mnene anza mazoezi upunguze unene.
 
Miaka 29 mm ni jinsia ya kike

tathimi menstruation cycle yako kama inaenda sawa, muda ambao kinakupata, pia kimeanza lini, ukihisi kasoro yoyote mwone dokta wa magonjwa ya wanawake.
 
Back
Top Bottom