THE GREAT CAMP
JF-Expert Member
- Jun 29, 2012
- 765
- 194
Nadhani hayo maneno Kinyama,Kishenzi na Kinoma ni maeneo ilikonyesha mvua
Duuuuuh asante.
Maeno haya ni misimu(maneno ambayo sio rasmi yanayotumika katika jamii fulani) watu wanaofaham maana ya maneno hayo ndio wanaoweza kuelewana...maana ya maneno hayo(kwa jinsi yalivyotumika) yanamaanisha sana(yaani mvua ilinyesha sana)
Duh,Nadhani hayo maneno Kinyama,Kishenzi na Kinoma ni maeneo ilikonyesha mvua
Maeno haya ni misimu(maneno ambayo sio rasmi yanayotumika katika jamii fulani) watu wanaofaham maana ya maneno hayo ndio wanaoweza kuelewana...maana ya maneno hayo(kwa jinsi yalivyotumika) yanamaanisha sana(yaani mvua ilinyesha sana)
kitaalamu hali hii tunaita UMILISI WA LUGHA wa mzungumzaji.Umilisi ni ile hali ya kuweza kuzalisha misamiati mingi au maneno mengi katika lugha anayoizungumza kwa umahili na mwenye uwezo wa kumkosoa mzungumzaji mwingineLeo nimekutana na watu njiani wanazungumza maneno yafuatayo kwenye simu: " Nasikia huko nyumbani Mvua inanyesha KINYAMA, wee Juzi ndiyo ilinyesha KISHENZI, nasikia na kijiji cha jirani imenyesha KINOMA"
Nikawa najiuliza.
1. Mvua inanyesha KINYAMA?
2.Mvua inanyesha KISHENZI?
3.Mvua inanyesha KINOMA?
Nini maana yake; maana kwenye Jiografia nimetafuta maana nimekosa. Naomba wale wataalamu wa Kiswahili mnisaidie.
Nadhani hayo maneno Kinyama,Kishenzi na Kinoma ni maeneo ilikonyesha mvua
Duuuuh we mtaalamu kwelikweli. Nashukuru sana, wengine kiswahili tunazungumza tuu lakini utaalamu wake hatuna. Ahsante sana.kitaalamu hali hii tunaita UMILISI WA LUGHA wa mzungumzaji.Umilisi ni ile hali ya kuweza kuzalisha misamiati mingi au maneno mengi katika lugha anayoizungumza kwa umahili na mwenye uwezo wa kumkosoa mzungumzaji mwingine
endapo kakosea katika mazungumzo.Kwa mtazamo wangu maneno haya yote yana maana sawa ya kwamba Mvua ilinyesha kwa wingi,ingawa maneno yanatofautiana kimaumbo ili tu kuonyesha kiwango cha Mvua kuzidi sehemu nyingine.
Imeandaliwa na bwana:Mbwilo,S.(2013).
Nimeipenda hii.sifa ya BAKITA,TUKIkuliingiza neno kwenye kamusi sio suala la kuamua na kufanya wao kama wao.hapa ni lazima msamiati huo kuweza kutumika na watu wengi kijiografia na lkiwa na maana sawa katika matumizi,hivyo neno kinyama,kishenzi,na kichizi ni maneno ambayo saana hutumiwa na vijana hasa wa mitaani ambao katika mazungumzo yao mara nyingi sikuhizi huingiza hata matusi kwenye mazungumzo.Na haya maneno kwa uhalisia ni vivumishi,ila yanakaa kama kielezi.:smiling::smiling:😛op2:
Mimi ndiyo nilikuwa nakimbia kabisa darasani wakati wa kipindi cha kiswahili nikiwa O'level. Kiukweli nilibahatisha kufaulu, maana kuna mambo kwenye kiswahili nyie acheni.Wanasema hesabu ngumu mi nakataa kiswahili ndo kigumu.