Msaada tafadhari: Kwa mnaojua kiswahili fasaha

THE GREAT CAMP

JF-Expert Member
Joined
Jun 29, 2012
Posts
765
Reaction score
194
[h=5]Leo nimekutana na watu njiani wanazungumza maneno yafuatayo kwenye simu: " Nasikia huko nyumbani Mvua inanyesha KINYAMA, wee Juzi ndiyo ilinyesha KISHENZI, nasikia na kijiji cha jirani imenyesha KINOMA"
Nikawa najiuliza.
1. Mvua inanyesha KINYAMA?
2.Mvua inanyesha KISHENZI?
3.Mvua inanyesha KINOMA?

Nini maana yake; maana kwenye Jiografia nimetafuta maana nimekosa. Naomba wale wataalamu wa Kiswahili mnisaidie.[/h]
 
Nadhani hayo maneno Kinyama,Kishenzi na Kinoma ni maeneo ilikonyesha mvua
 
Hicho ni kiswahli cha mtaani kijana.
 
Maeno haya ni misimu(maneno ambayo sio rasmi yanayotumika katika jamii fulani) watu wanaofaham maana ya maneno hayo ndio wanaoweza kuelewana...maana ya maneno hayo(kwa jinsi yalivyotumika) yanamaanisha sana(yaani mvua ilinyesha sana)
 
Kama ni hivyo itabidi tuwaombe BAKITA au TUKI waingize maneno hayo kwenye kamusi.
 
sifa ya BAKITA,TUKIkuliingiza neno kwenye kamusi sio suala la kuamua na kufanya wao kama wao.hapa ni lazima msamiati huo kuweza kutumika na watu wengi kijiografia na lkiwa na maana sawa katika matumizi,hivyo neno kinyama,kishenzi,na kichizi ni maneno ambayo saana hutumiwa na vijana hasa wa mitaani ambao katika mazungumzo yao mara nyingi sikuhizi huingiza hata matusi kwenye mazungumzo.Na haya maneno kwa uhalisia ni vivumishi,ila yanakaa kama kielezi.:smiling::smiling:😛op2:
 
Maeno haya ni misimu(maneno ambayo sio rasmi yanayotumika katika jamii fulani) watu wanaofaham maana ya maneno hayo ndio wanaoweza kuelewana...maana ya maneno hayo(kwa jinsi yalivyotumika) yanamaanisha sana(yaani mvua ilinyesha sana)

Wala hiyo si misimu ni lugha ya kihuni,misimu ni lugha inayozuka na kutoweka miongoni mwa jamiifulani na huweza kusanifisha na kuwa lugha sanifu sasa hiyo kishenzi na kinyama unaweza kusanifisha
 
Leo nimekutana na watu njiani wanazungumza maneno yafuatayo kwenye simu: " Nasikia huko nyumbani Mvua inanyesha KINYAMA, wee Juzi ndiyo ilinyesha KISHENZI, nasikia na kijiji cha jirani imenyesha KINOMA"
Nikawa najiuliza.
1. Mvua inanyesha KINYAMA?
2.Mvua inanyesha KISHENZI?
3.Mvua inanyesha KINOMA?

Nini maana yake; maana kwenye Jiografia nimetafuta maana nimekosa. Naomba wale wataalamu wa Kiswahili mnisaidie.
kitaalamu hali hii tunaita UMILISI WA LUGHA wa mzungumzaji.Umilisi ni ile hali ya kuweza kuzalisha misamiati mingi au maneno mengi katika lugha anayoizungumza kwa umahili na mwenye uwezo wa kumkosoa mzungumzaji mwingine
endapo kakosea katika mazungumzo.Kwa mtazamo wangu maneno haya yote yana maana sawa ya kwamba Mvua ilinyesha kwa wingi,ingawa maneno yanatofautiana kimaumbo ili tu kuonyesha kiwango cha Mvua kuzidi sehemu nyingine.

Imeandaliwa na bwana:Mbwilo,S.(2013).
 
Wanasema hesabu ngumu mi nakataa kiswahili ndo kigumu.
 
Duuuuh we mtaalamu kwelikweli. Nashukuru sana, wengine kiswahili tunazungumza tuu lakini utaalamu wake hatuna. Ahsante sana.
 
sifa ya BAKITA,TUKIkuliingiza neno kwenye kamusi sio suala la kuamua na kufanya wao kama wao.hapa ni lazima msamiati huo kuweza kutumika na watu wengi kijiografia na lkiwa na maana sawa katika matumizi,hivyo neno kinyama,kishenzi,na kichizi ni maneno ambayo saana hutumiwa na vijana hasa wa mitaani ambao katika mazungumzo yao mara nyingi sikuhizi huingiza hata matusi kwenye mazungumzo.Na haya maneno kwa uhalisia ni vivumishi,ila yanakaa kama kielezi.:smiling::smiling:😛op2:
Nimeipenda hii.
 
Wanasema hesabu ngumu mi nakataa kiswahili ndo kigumu.
Mimi ndiyo nilikuwa nakimbia kabisa darasani wakati wa kipindi cha kiswahili nikiwa O'level. Kiukweli nilibahatisha kufaulu, maana kuna mambo kwenye kiswahili nyie acheni.
 
Back
Top Bottom