Msaada tafadhari kwa wanandoa na madkt

jamii01

JF-Expert Member
Joined
Oct 1, 2010
Posts
1,983
Reaction score
1,423
Mke wangu kajifungua baada ya mda mfupi mtoto akawa amefariki uzao wa kwanza,kwa sasa yuko nyumbani anaendelea vyema,napenda kujua natakiwa kukaa kwa mda gani kama hatujaanza kukutana tena kimwili kama wanandoa?sina uzoefu wowote ule naomba nisaidiwe.
 
pole sana, mi napita ila wakija kina Mzizimkavu,asprin, king'ast, madam X, na wengineo watakusaidia,..
 
asante,ngaoja niwasubiri
 
Siku 42 tu, kipindi cha puperium kinakuwa kimekwisha, hata zile damu damu zinakuwa zimekwisha, hii ni kwa mwanamke yeyote yule aliyezaa.
Nawatakia kila la kheri, ila kabla hamjaanza kutafuta mtoto mwone Dr ili mjue nini sababu ya mtoto kufa, ili mfanye maandalizi isijirudie tena uzao ujao.
 
poleni sana wewe pamoja na mkeo.ni vizuri kumpa mkeo muda maana jambo la kufiwa na mtoto pengine yeye mwenyewe atakuwa na machungu yake.inshallah mtakapokuwa tayari mtapata mtoto mwengine
 
poleni sana, Dr Mzizi Mkavu pls where r u?
Mkuu Tusker Bariiiidi Amesha jibu mkuu.@Mupirocin Ni Siku 42 tangu alipozaa na mtoto wake kufariki hata kwa ndugu zetu Waislam huwa wanafanya hivyo ukizaa na mtoto akifariki inatakikana mwanamke akae siku 40 ndio anaweza kufanya tena tendo la mapenzi au kutafuta mtoto mwengine.
 
Last edited by a moderator:
Aisee, poleni sana kaka.
Nikutahadharishe kuwa mwanamke akiwa na matatizo ya kihisia, mara nyingi kujamiina (kwa maana ya socialising) inamuwia ngumu kweli kweli. Kuna vipindi atahitaji kukaa mwenyewe na kulia. Ni sehemu ya kupona, isikushtue. Tofauti na mwanaume ambae sex inamuondolea stress, mwanamke anakosa kutamani sex akiwa na stress.

Kama ulivyoambiwa, 40 ikipita unaweza kuendelea. Lakini nakusihi umpe mwenzako nafasi ya kupona kihisia kwa kuwa rafiki yake. Jitahidi umuelewe, hii itakuweka karibu nae na kuwafanya muwe sawa haraka. Inshaallah Mungu wa rehema atarudisha kila lililoibiwa na mwovu.
 
Nashukuruni sana kwa msaada wenu...
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…