Aisee, poleni sana kaka.
Nikutahadharishe kuwa mwanamke akiwa na matatizo ya kihisia, mara nyingi kujamiina (kwa maana ya socialising) inamuwia ngumu kweli kweli. Kuna vipindi atahitaji kukaa mwenyewe na kulia. Ni sehemu ya kupona, isikushtue. Tofauti na mwanaume ambae sex inamuondolea stress, mwanamke anakosa kutamani sex akiwa na stress.
Kama ulivyoambiwa, 40 ikipita unaweza kuendelea. Lakini nakusihi umpe mwenzako nafasi ya kupona kihisia kwa kuwa rafiki yake. Jitahidi umuelewe, hii itakuweka karibu nae na kuwafanya muwe sawa haraka. Inshaallah Mungu wa rehema atarudisha kila lililoibiwa na mwovu.