Msaada: Tafsiri ya ndoto hii

Msaada: Tafsiri ya ndoto hii

JOSEPH JOEL

Member
Joined
May 18, 2012
Posts
14
Reaction score
3
Usiku wa kuamkia leo nimeota mchumba wangu kachelewa kurudi nyumbani akadai ameogopa kunigongea ningempiga na akaenda kulala dukani kwani aliniaga anaenda kwenye party nikamruhusu

Baada ya muda panatokea maaskari na mgambo dukani wakidai wanamuulizia binti anaitwa Saada ambaye inasadikika alikuwa na mwanaume kutoka South Afrika kwa muda mrefu lodge ya mtaani hapo ila huyo mwanaume amekufa muda mrefu na ameoza na funza zinamtoka mwilini,

kwahiyo Serikali ikaamulu tumzikie hapo mtaani kama wana mtaa kushirikiana na uongozi wa mtaa wakati wa mazishi mchumba wangu akaubeba mwili kuelekea makaburini tukiwa njiani akuacha ili mtu mwingine ampokee lakini yule mtu akauangusha chini kutokana na harufu na funza wengi sana kwa ujasiri mchumba wangu akauchukua tena ule mwili akaubeba hadi makaburini ukazikwa

Wakati tunarudi palikuwa na ndoo ya kunawa mikono mchumba akaanza kunawa akawa anaondoka baada ya mimi kunawa nikamuona tayari ametangulia nikaanza kumkimbilia huku namuita ili tuongozane maana alikuwa anaelekea dukani tena akafika umbali wa kona ambao sikuweza kumuona nikakutana na mtu tukasalimiana tu.

Na nikashtuka usingizini.

Msaada wa tasfiri ya ndoto hii kwa wajuzi.
 
Achana mara moja na huyo mchumba wako Saada.

Usipofanya hivyo mapema, basi usije kujilaumu hapo baadaye.
 
Funza, uchawi wa funza upo malawi na tunduma huko.

Ngoja tuone pengine dada anataka akachukue mzigo huko, ngoja tutamuuliza hamfureyi
 
Usiku wa kuamkia leo nimeota mchumba wangu kachelewa kurudi nyumbani akadai ameogopa kunigongea ningempiga na akaenda kulala dukani kwani aliniaga anaenda kwenye party nikamruhusu

Baada ya muda panatokea maaskari na mgambo dukani wakidai wanamuulizia binti anaitwa Saada ambaye inasadikika alikuwa na mwanaume kutoka South Afrika kwa muda mrefu lodge ya mtaani hapo ila huyo mwanaume amekufa muda mrefu na ameoza na funza zinamtoka mwilini,

kwahiyo Serikali ikaamulu tumzikie hapo mtaani kama wana mtaa kushirikiana na uongozi wa mtaa wakati wa mazishi mchumba wangu akaubeba mwili kuelekea makaburini tukiwa njiani akuacha ili mtu mwingine ampokee lakini yule mtu akauangusha chini kutokana na harufu na funza wengi sana kwa ujasiri mchumba wangu akauchukua tena ule mwili akaubeba hadi makaburini ukazikwa

Wakati tunarudi palikuwa na ndoo ya kunawa mikono mchumba akaanza kunawa akawa anaondoka baada ya mimi kunawa nikamuona tayari ametangulia nikaanza kumkimbilia huku namuita ili tuongozane maana alikuwa anaelekea dukani tena akafika umbali wa kona ambao sikuweza kumuona nikakutana na mtu tukasalimiana tu.

Na nikashtuka usingizini.

Msaada wa tasfiri ya ndoto hii kwa wajuzi.
🤣🤣🤣🤣🤣🤣
Ndoto tu mkuu..nothing serious
 
Back
Top Bottom