Msaada: tatizo la damu kuviria tumboni

future mind

JF-Expert Member
Joined
Dec 13, 2016
Posts
221
Reaction score
229
Wakuu natumaini mu wasima...niwape pole sana ndugu zangu waliopotelewa na jamaa zao katika ajali ya MV Nyerere poleni sana mungu awajalie nguvu ya uvumilivu katika kipindi ichi kigumu.

Bila kupoteza mda niende moja kwa moja kwenye mada kama nilivyoeleza hapo juu hivi majuzi nimekuwa nikiumia sana kuona rafiki yangu akiteseka na maumivu makali nimekuwa nikiwaza ni jinsi gani yakumsadia nashindwa kujua nianzie wapi ili kumsaidia hili tatizo limeanza kuwa serious kwake hivi majuzi huu ni mwezi wa nne sasa akiteseka na maumivu alienda hospital nakufanyiwa ultrasound ikaonekana kuna tatizo la damu imeviria tumboni.

Chakushangaza zaidi pia mguu umekuwa ukimuuma sana mguu wa upande ule ule ambapo tumboni kuna tatizo ambalo vipimo vinaonyesha ni karibu na nyonga.

Hospital walimwandikia dawa zakumeza yaani vidonge vyakutumia kwa kipindi cha miezi mitatu hadi sasa anamalizia mwezi wa pili ila anasema haoni nafuu yoyote maumivu ni yale yale yaani akitembea tu kidgo anapata maumivu pia akikaa kwa mda pia anasikia paja linamuuma, naona kama anapoteza matumaini.

Msaada wenu wakuu wa mawazo ushauri ni nini afanye maana pia anasema ataki kwenda tena hospital, naomba kama kuna mtu amewai kusikia tatizo kama ili au anajua tiba yake ..pia ushauri wenu wataalam ni humu sana.

NB: ajawai kupata ajali na wala kupigwa maeneo hapo ya tumbo.
~Asanteni na mungu awabariki sana,~
 
Aiseee pole nyingi kwake kina dk mwaka wanakuja
 
Asante kwa niaba mkuu ngoja tuendelee kuwasubiria,
 
Maelezo hayo hayajitoshelezi hata kidogo na bado yana ukakasi, kwa kipimo alichofanya na majibu aliyopewa. Nisihoji sana, ila wewe mshauri kwenda hospitali nyingine maana hakuna matibabu ya namna hiyo kwa tatizo unaloeleza labda kama kuna taarifa haijakaa sawa.
 
Kweli mkuu nimerudia kumuuliza vizuri ila me ndio nilichanganya kasema alifanya ultrasound na sio exray kama nilivyoeleza,
 
Alikuwa anatibiwa wapi? Dawa zipo anatumia
Mkuu kwa sasa sipo nae karibu sana yani kahama alipokuwa anakaa ila naenda kumtembea siku sio nyingi nitakuja na majibu,
 
Kweli mkuu nimerudia kumuuliza vizuri ila me ndio nilichanganya kasema alifanya ultrasound na sio exray kama nilivyoeleza,

Si unaona anavyibadili badili maelezo. Afanye tu kwenda hospitali tofauti na alivyoenda mwanzo asisubiri azidiwe
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…