Msaada: Tatizo la kutosikia vizuri

Msaada: Tatizo la kutosikia vizuri

Kwa kifupi masikio ishu complicated sana sio bongo tu duniani kote ukipata taizo la kusikia jikubali tu ngumu sana kurudi kama zamani
Ipo hivyo mkuu, na uking'ang'ania tu lazima upigwe hela ndefu hadi uchakae. Anyway sikatishi mtu tamaa ila kila mmoja ajaribu matibabu kwa imani yake.
 
mimi naamini bado hii shida ya masikio ina dawa tena mtu unapona kabisa. kuna jamaa namfahamu alikuwa na hii shida miaka kibao uko nyuma. Tulipoteana miaka mingi na kukutana mwaka jana naona yupo fresh ana usikivu mzuri tu ila bahati mbaya sikupata wasaa nimdodose alifanyaje au aliponea wapi.

kwa mtazamo wangu hili tatizo la kutosikia linachangiwa pia na wahusika kuchelewa kupata matibabu. Watu wengi pale mwanzo wanakuwa ni kama hawajijui kama wana hiyo shida. ila sasa wewe uliye karibu ndo unaweza kujua au kuhisi uyu jamaa ana tatizo la kusikia. shida sasa ukimwambia mtu ukweli ndo mnaanza kubishana na wengine hata ngumi zinaweza kurushwa.

ishu ingine nayoiona saivi hasa kwa mateen wengi ni matumizi ya spika za masikio "headphones". tena wengi wao hupandisha sauti hata mtu uliyembali unaweza kusikia vizuri tu. matumizi ya hizi spika za masikio tena kwa sauti za juu ni janga lingine la kuharibu masikio.
 
Nil
Habarini ndugu zangu.

nna mchumba wangu anatatizo la kutosikia vizuri,hali hii imemtokea tu ivi karibuni zamani hakuwa na tatizo hili hata kidogo,

shida ilianza pale alipoenda field pale idara ya maji mwanza, kwa maelezo yake alikuwa kwenye kitengo cha kutibu maji,sasa humo kuna mashine zinaunguruma sana na walikuwa hawapewi headphones (labda walidharauliwa sababu ni wanafunzi wako tu field).

sasa toka aondoke masikio yake hayasikii vizuri hadi uongee kwa sauti, kaenda hospital kaambiwa ngoma za masikio zimeingia ndani kapewa dawa nyingi kinoma kameza zote lakini hali bado.

nmempeleka kwa waganga wa kienyeji kaambiwa eti kuna mwenzie kamroga asifaulu chuo kampa madawa kanywa hadi kachoka,chale za kutosha, n.k.

Ana miezi sita saiv tatzo bado.

Ushauri na msaada anayejua zaid juu ya hili tatizo anisaidie.
Nilienda KCMC nikapimwa nikagundulika tatizo ni mishipa ya fahamu iliachana . Nilishawahi kung'olewa jino ukubwani. Lilinisababishia matatizo. Ninayo vifaa kwasasa. Nafanya kazi kama Kawa.
 
Kiongozi naomba nipate mawasiliano yako, natumai naweza kupata msaada na ushauri kwako
 
Back
Top Bottom