MSAADA: Tiba ya tatizo la kutoona mbali.

Wisest man

JF-Expert Member
Joined
Jul 29, 2013
Posts
993
Reaction score
332
Mdogo wangu haoni mbali na matatizo hayo yalianza miaka 13 alipewa dawa za hospital za kuweka kwenye macho lakini wapi! akaenda ccbrt wakamcheki wakamwambia kuwa hana matatizo yanahitaji upasuaji, akashauriwa atumie miwani na awe anakula mbogamboga na matunda, lakini tatizo la kutosikia vizuri nalo likajitokeza sasa anatafuta tiba za vidonge asili, amekuwa na mashaka ya kutopona kwa sababu hata dawa za hospital hazikumsaida. je ataweza kupona kwa tiba asili na wapi pana tiba ya uhakika? na gharama yake je?
 
Tatizo la dogo ni kwamba anachagua vyakula, kwa mf. hataki kula baadhi mboga kama dagaa, spinachi,mchicha, hivyo nikaona ni bora apate tiba ya vidonge moja kwa moja, aliwahi kushauriwa na dr.mmoja hivyo ila anapuuza, kwani alikuwa akivaa miwani anajiona tayari amepona.
 
Mpeleke Hospitali ya Muhimbili kuna wataalam wazuri na wapo pia Waganga wa Tiba za asilia anaweza kupona inshallah........

MziziMkavu njoo umpe huyu mwenzetu dozi zako za mizizi.
Mkuu Jamaa_Mbishi Hali yako?
 
Last edited by a moderator:
Pole lakini;
Pamoja na kushauriwa ale mbogamboga anaonekana pia hapendi,
Inawezekana hata dawa hamezi na badala yake anazitupia hukooo mbali.

Mpe tu ushauri kuwa ni muhimu kufuata ushauri wa daktari;
vinginevyo yatamkuta ya sikio la kufa halisikii dawa.

..................Pole sana.
 
Mkuu hali yangu shwari tu, ulikuwa wapi waziri mteule? Jamaa hapo juu anahitaji msaada wako.
Kama alivyoshauriwa na Doctor apendelee kula sana matunda na mboga mboga na samaki kama ni mtoto mdogo macho yake yatarudi kuwa mazuri huenda pia ana upungufu wa Vitamin mwilini ndio maana nimempa ushauri aende Hospitali kuu ya muhimbili kuna Wataalam zaid wa masuala ya macho . kuliko kungojea hapa ushauri wa watu humu ndani.

MziziMkavu yaani umechoka kiasi cha kututuma muhimbili jamani?
Mzima lakini.
Sijachoka nimechoka na hizi kesi Mdogo wangu anaumwa na macho,shemaji yangu anaumwa ana tumbo, kaka

yangu anaumwa na miguu, mke wangu ana umwa kiuno kwanini husemi ni wewe ninaye umwa ili tupate kukuliza maswali kuhusu

ugonjwa wako? unamsingizia mtu ambaye hata kumwa haumwi hata kidogo, kwani ukisema jamani mimi ninaumwa maradhi fulani ?

Unamuogopa nani kusema matatizo ya kwako uliyo nayo?
 

Mkuu pole sana hata mimi pia mdogo wangu macho yalianza kumsumbua ghafla yaani haoni mbali akiwa darasani hawezi kuyaona maandishi ya ubaoni nilimpeleka hospital ya mkoa Iringa hawakuweza kuona tatizo wakanishauri nimpeleke CCBRT pale napo madaktari walifanya kila aina ya vipimo hawakuona tatizo wakaniandikia baadhi ya vipimo nikachukue mhimbili nako tatizo halikuonekana nikashauriwa nimpeleke south Africa hapo ndo mambo yalivoanza kuwa magumu kwa sababu uwezo ulikua hafifu ila wakanishauri naweza kutumia maagent ambao wapo hapo mhimbili au Regency kwa sababu Regency ilikua wakichukua sample baada ya weeks 2 majibu yanakua tayari nili2mia Regency majibu yakawa yaleyale hakuna ugonjwa hadi Sasa nimechanganyikiwa Mkuu naomba kama utapata ufumbuz wa tatizo lako naomba nami nijulishe nakuinbox namba yangu.
 
Mwambie huyo mdogo wako atumie vyakula hivi kila siku vitamsaidia kupona hayo Macho yake.

 

Attachments

  • VYAKULA KWA AJILI YA MACHO YAKO.jpg
    76 KB · Views: 866
Dah! Tatizo kama langu ila sina uwezo wowote labda atokee mtu anisaidie sioni mbali SIKIO 1 alifanyi kazi ila napokea ushauri kwa yoyote nini nifanye nipate nafuu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…