Aisee nimependa hili Swali.Kisha utamuuliza wakati anakuona alitumia darubini? Maana kumwona mtu aliyeko Mwanza akimtishia kumkata mtu panga wa Dar wakati mtkataji panga 6 akiwa Mwanza yataka uwe na darubini. Na hilo panga yaelekea ni aiba ya kombora maana panga kutoka Mwanza mpaka Dar ili liweze kumkata mtu linahitaji mtambo wa kurushia kombora.
Sent using Jamii Forums mobile app
Wastage of time. Usiwaulize hilo swali maana utakuwa katika disadvantage. Ukiuliza swali hilo kisha mtu akajibu anakujua maana aliwahi kukukuta ukigombana na mtu ama ukipigana na mtu utajiweka pabaya hata kama anakusingizia. Utaonekana una asili ya ukorofi na ugomvi hivyo kuku link na tukio la kutishia kwa panga.Nashukuru Mr Malyenge, umenipatia jibu zuri sana anbalo naweza kulitumia siku ya kesi. Pia naomba maswali zaid ninayoweza kuuliza siku hiyo. Pia nilipanga kuuliza mashahidi kama wananifahamu na ni kwa muda gani wananifahamu na wananifahamu kama nani, je niswali sahihi la kuuliza???
Sent using Jamii Forums mobile app
Usiulize hilo suala utajikaanga...Je kama nikiuliza ni kitu gan kilimnusuru nisitekeleze azma ya kumkata ni sawa?? Pia nikimuuliza shahid kuwa alichukua hatua gan baada ya kuona haya yote nitakuwa sawa ??
Sent using Jamii Forums mobile app
Hapana mkuu Malyenge, kutoa defence ya kutokuwepo inaitwa ALIBI kanuni zinataka ukitaka kutoa defence hii lazma utoe taarifa (notice) kuwa uta_rise a defence of alibi (km ilivyo kwny P.O) cannot be raised by surprise. So ni sahihi kutoa taarifa kabla.Wakati wa kujitetea ndio useme hukuwapo. Achana na kusema hukuwapo kabla haijafika zamu yako ya kujitetea. Watauhujumu utetezi wako.
Sent using Jamii Forums mobile app
Inanikumbusha kesi ya Kamando ChisimaPole sana na pia pongezi kwa wote mliotoa msaada na ushauri. Ila hapo unachokizungumza mleta mada kwenye sheria inaitwa defense ya alibi (inasomeka alabai au alibi hivyohivyo). Hii ni defense kuonesha kuwa siku ya tukio hukuwepo eneo la tukio, ili itumike mahakamani ni lazima uutaarifu mapema (kwa maandishi) upande wa pili kuwa unakusudia kutumia hiyo defense ya alibi..
Sababu kuu ya kuwataarifu ni hii; tofauti na wengi walivyosema kuwa ukaombe manifest kwenye kampuni ya basi nk kuthibitisha kutokuwepo kwako, kisheria upande wa pili ndio wanaotakiwa kuthibitisha kuwa ulikuwepo eneo la tukio wakati tukio likifanyika na sio wewe kuthibitisha kuwa hukuwepo eneo hilo.. Hivyo unawapa taarifa ili wajiandae kuthibitisha kuwa ulikuwepo eneo la tukio.. Ni muhimu lakini kuwa na tiketi na vielelezo vingine (kama hiyo manifest nk)