Jicholamwewe
JF-Expert Member
- Jan 2, 2021
- 374
- 473
CCM hoyeeeWaheshimiwa, habari ya kazi na pole kwa majukumu.
Waheshimiwa, mwaka jana 2023, nilibahatika kupata ufadhili wa kwenda masomoni nje ya nchi hivyo nililazimika kutafuta passport. May 2023, nilifika ofisi za uhamiaji Kurasini na viambatanisho vyangu vyote kufanya ombi la passport. Nilifanikiwa kukamilisha ombi langu na kulipia gharama zote.
Waheshimiwa, toka May 2023, hadi sasa sijapata passport. Nilipojaribu kufatilia niliambiwa siwezi kupata passport kwa sababu mimi sio Mtanzania.
Waheshimiwa, mimi nimezaliwa, kukua na kusoma ndani ya mipaka ya Tanzania kama viambatanisho vyangu vinavyoonyesha. Wazazi pamoja na babu zangu ni watanzania.
Waheshimiwa, nimefanya jitihada zote pamoja na kuleta wazazi kutoka kijijini na kwenda nao uhamiaji bila mafanikio. Nimeingia gharama kubwa sana kufuatilia hili swala ukizingatia mimi ni kijana niliyemaliza chuo na bado sijabahatika kupata kazi. Kadhalika kuna uwezekano nikapoteza ufadhili niliobahatika kuupata kama sitapata passport kwa wakati; ndoto na maisha yangu kiujumla yataharibika kwani elimu ndio tegemeo langu kujikwamua kiuchumi.
Waheshimiwa nimekuwa ni MTU wa mawazo sana pamoja na misongo. Naombeni msaada wenu kutokomeza ukosefu wa haki katika nchi hii.
Ni mimi kijana mwenzenu Mwenyezi Mungu awabariki mnapoendelea na majukumu ya ujenzi wa taifa.
hela tenaaaPole sana ,mim nilihangaika sana kupata hapa Mwanza nikaombwa hadi rushwa ya ngono nikakataa nikasema kama kupata passport ni kazi hivi basi siitaki,
nikapata kazi Dodoma nikaomba migration ya Dodoma nikaunganishwa na baba mmoja hivi hapo Migration hakuniomba chochote niliombwa Doc za sababu ya kusafiri G akanitumia barua ya mwaliko na passport copy yake ndani ya wiki mbili nikapata passport ,nikasema nimpe asante yule baba aliikataa kata kata akasema nimekusaidia tu
Tafuta mtu akuunganishe utaipata haraka tu
Sasa ili wakuthibitishe Kuwa wewe ni Mtanzania unatakiwa uwapelekee Tunu kadhaa za Taifa ambazo ni currencies za kitanznia (Fedha halali) ili waamini kweli wewe ni mtanzania..Waheshimiwa, habari ya kazi na pole kwa majukumu.
Waheshimiwa, mwaka jana 2023, nilibahatika kupata ufadhili wa kwenda masomoni nje ya nchi hivyo nililazimika kutafuta passport. May 2023, nilifika ofisi za uhamiaji Kurasini na viambatanisho vyangu vyote kufanya ombi la passport. Nilifanikiwa kukamilisha ombi langu na kulipia gharama zote.
Waheshimiwa, toka May 2023, hadi sasa sijapata passport. Nilipojaribu kufatilia niliambiwa siwezi kupata passport kwa sababu mimi sio Mtanzania.
Waheshimiwa, mimi nimezaliwa, kukua na kusoma ndani ya mipaka ya Tanzania kama viambatanisho vyangu vinavyoonyesha. Wazazi pamoja na babu zangu ni watanzania.
Waheshimiwa, nimefanya jitihada zote pamoja na kuleta wazazi kutoka kijijini na kwenda nao uhamiaji bila mafanikio. Nimeingia gharama kubwa sana kufuatilia hili swala ukizingatia mimi ni kijana niliyemaliza chuo na bado sijabahatika kupata kazi. Kadhalika kuna uwezekano nikapoteza ufadhili niliobahatika kuupata kama sitapata passport kwa wakati; ndoto na maisha yangu kiujumla yataharibika kwani elimu ndio tegemeo langu kujikwamua kiuchumi.
Waheshimiwa nimekuwa ni MTU wa mawazo sana pamoja na misongo. Naombeni msaada wenu kutokomeza ukosefu wa haki katika nchi hii.
Ni mimi kijana mwenzenu Mwenyezi Mungu awabariki mnapoendelea na majukumu ya ujenzi wa taifa.
Hahahahaha! Mkuu nimecheka sana..Sasa ili wakuthibitishe Kuwa wewe ni Mtanzania unatakiwa uwapelekee Tunu kadhaa za Taifa ambazo ni currencies za kitanznia (Fedha halali) ili waamini kweli wewe ni mtanzania..
Vinginevyo hutaweza kupata unachokitaka
Eee kama shukran tu sijahangaikahela tenaaa
ngono tenaaaaa
mmmh