Msaada: Toka May 2023 hadi sasa sijapata passport, nimeambiwa mimi sio mtanzania

Msaada: Toka May 2023 hadi sasa sijapata passport, nimeambiwa mimi sio mtanzania

Waheshimiwa, habari ya kazi na pole kwa majukumu.

Waheshimiwa, mwaka jana 2023, nilibahatika kupata ufadhili wa kwenda masomoni nje ya nchi hivyo nililazimika kutafuta passport. May 2023, nilifika ofisi za uhamiaji Kurasini na viambatanisho vyangu vyote kufanya ombi la passport. Nilifanikiwa kukamilisha ombi langu na kulipia gharama zote.

Waheshimiwa, toka May 2023, hadi sasa sijapata passport. Nilipojaribu kufatilia niliambiwa siwezi kupata passport kwa sababu mimi sio Mtanzania.

Waheshimiwa, mimi nimezaliwa, kukua na kusoma ndani ya mipaka ya Tanzania kama viambatanisho vyangu vinavyoonyesha. Wazazi pamoja na babu zangu ni watanzania.

Waheshimiwa, nimefanya jitihada zote pamoja na kuleta wazazi kutoka kijijini na kwenda nao uhamiaji bila mafanikio. Nimeingia gharama kubwa sana kufuatilia hili swala ukizingatia mimi ni kijana niliyemaliza chuo na bado sijabahatika kupata kazi. Kadhalika kuna uwezekano nikapoteza ufadhili niliobahatika kuupata kama sitapata passport kwa wakati; ndoto na maisha yangu kiujumla yataharibika kwani elimu ndio tegemeo langu kujikwamua kiuchumi.

Waheshimiwa nimekuwa ni MTU wa mawazo sana pamoja na misongo. Naombeni msaada wenu kutokomeza ukosefu wa haki katika nchi hii.

Ni mimi kijana mwenzenu Mwenyezi Mungu awabariki mnapoendelea na majukumu ya ujenzi wa taifa.
Mtu muhimu sana kwenye uraia wako ni mama yako na bibi yako, taarifa za mama yako yaani jina lake kamili na aliko kuzalia, yaani yeye ni mtanzania alikuzalia Kenya ujue wewe si mtanzania ukishindwa hapo basi pasipoti utaisikia tu.
 
Pole, Natamani ningekusaidia, ila nina uhakika utapata usaidizi wa haraka hapa hapa JF
 
Oh sawa twanzie hapo walipokwambia we si mtanzania
nataka kufahamu haya
  1. Umezaliwa mkoa gani
  2. Kabila lako
  3. Umesoma shule ya msingi ipi kwa jina na iliyopo mkoa gani na wilaya.
  4. Wazazi wako wapo wapi.
Hebu jibu kwanza haya then tuone njia ipi itafunguka
1.Morogoro
2.Mha
3.Shule ipo Morogoro wilaya kilosa
4.wazazi sasa wapo Morogoro.walitoka kigoma 1992 kuja Morogoro
 
In
Nikweli wazazi wanatokea kigoma. Mimi nimezaliwa moro
Kuna jamaa tulikuwa naye jeshini alikoswa kazi kisa katoka kigoma,na lisura lake lilifananishwa na warundi,alirudi home kabisa hadi leo anasota uraiani.


Kama ni kigoma ni changamoto sana,hakuna namna,omba kwa imani yako Mungu akusaidie,by the way wakati mwingine mambo yako yakienda tofauti na unavyofikiri hupaswi kujuta sana,kuna kitu nature inataka kukusave nacho.
 
Pole sana, mimi nilihangaika sana kupata hapa Mwanza nikaombwa hadi rushwa ya ngono nikakataa, nikasema kama kupata passport ni kazi hivi basi siitaki.

Nikapata kazi Dodoma nikaomba migration ya Dodoma nikaunganishwa na baba mmoja hivi hapo Migration hakuniomba chochote niliombwa Doc za sababu ya kusafiri, G akanitumia barua ya mwaliko na passport copy yake ndani ya wiki mbili nikapata passport, nikasema nimpe asante yule baba aliikataa kata kata akasema nimekusaidia tu.

Tafuta mtu akuunganishe utaipata haraka tu
Ulitaka kumpa asante ya kitu gani huyo Baba?

😎
 
Pole sana. Hao wanataka hela tu tafuta ofisa mmoja hapo uhamiaji jenga mazoea nae muelezee scenario ukimaliza kupiga ne story muachie Hela ya asante ili kuujenga ushkaji.

Mbona atakupambania na jambo lako pia inabidi ulitolee mpunga mwingine ili alifanikishe. Ndani ya Wiki mbili utapata.
 
Kuna mikoa Tz ukitaja tu utabanwa kama gaidi
Yaani hata bungeni hawataki kukemea
Labda umetokea mwisho wa nanihiii
 
Back
Top Bottom