Msaada: Toyota oppa imeanza matatizo baada ya kuifanyia service

Msaada: Toyota oppa imeanza matatizo baada ya kuifanyia service

Cipher op

Member
Joined
Jan 25, 2015
Posts
76
Reaction score
99
Msaada wenu wakuu gari yangu wiki iliyopita nimepeleka garage kuifanyia service. Service nilizofanya ni pamoja na kumwaga na kubadili oil na kubadili hydraulic na nyingine ndogondogo kazi ilifanyika vizuri kabisa. Tatizo limekuja baada ya kama Siku mbili kupita na tatizo lenyewe ni kama ifuatavyo
1.Nikiwasha gari inawaka lakini inatoa muungurumo kama machine ya dizel
2.Gari inawaka lakini nikiweka gia inazima
3.Nikitaka isizime basi ni lazima nikanyage kwenye kuongeza mwendo na haiwezi kumove
4.Nikiweka silence inazima yenyewe
NB: Gari ni Toyota oppa Auto na kabla ya service hiyo gari ilikuwa safi kabisa.
Msaada wenu wadau tatizo ni nini hasa na solution yake.
 
Sio mtaalamu sana ila ungesaidia basi kuongezea nyama hapo kwa kujibu haya maswali:

1.Toka ulimiliki umewahi fanya service kama izo mara ngapi na kwa fundi huyo huyo au?

2. Fundi "anaekufanyiaga" service umemuambia amesemaje?

Mengine watakuja wataalamu.
 
Kwajinsi ulivyoeleza,
Hio opa engine yake nahisi ni d-4.

Please comfirm.
 
service nilifanya mwaka Jana mwezi Wa Tisa mwaka jana
 
utakuwa ushakaanga engine, nahisi ulichanganya mafuta
Mafuta gani tena unayoongelea kaka? Ila ingekua tatizo la engine ingekua inawasha check engine light kwenye dashboard
 
Angalia plug zako kama zina choma!!! Cheki pump kama ina fanya kazi inavyotakiwa!!! Mwisho uwe unafanya service kwa wakati bosi!!! Na kwa fundi anaye eleweka!!!
 
Angalia plug zako kama zina choma!!! Cheki pump kama ina fanya kazi inavyotakiwa!!! Mwisho uwe unafanya service kwa wakati bosi!!! Na kwa fundi anaye eleweka!!!

Mimi namefanya once in a year (km 10,000 ila sio Tz), oil na filters zote ziko poa. Ishu nadhani sio timing ya muda bali kilometa na aina ya lubricants
 
Na mm nilikuwa na opa ikanifaniyia hivyo ebu ni pm nikwambie kitu
 
Sio mtaalamu sana ila ungesaidia basi kuongezea nyama hapo kwa kujibu haya maswali:

1.Toka ulimiliki umewahi fanya service kama izo mara ngapi na kwa fundi huyo huyo au?

2. Fundi "anaekufanyiaga" service umemuambia amesemaje?

Mengine watakuja wataalamu.
Tumia oil ya Bp,hiyo gari engine haitaki Petrol chafu. Safisha tank la mafuta kwanza
 
utakuwa ushakaanga engine, nahisi ulichanganya mafuta
Sina huakika na hilo coz Niko mkoa na sheli nayowekea mafuta in hiyo hiyo sijawai kubadili na huwa naweka Mara 1 au 2 kwa mwezi
 
Tatizo ndogo tu nimekuja inbox ebu nifate
 
Back
Top Bottom