Msaada: Toyota Voltz inakula mafuta lita moja kwa 7km

Zinakaa hata mwaka hasa kama Top Cover Gasket hailikishi oil kwenye coils kule maana huwa inaendaga kuua plug pre-maturely!

Tafta plug za Denso zinauzwa ghali kidogo ila ndio nzuri, mara ya mwisho mi niliweka nikaenda mbeya kwa mafuta ya 130K vizuri kabisa. Moshi to Dar nilishuka na Nusu Tank!
Hili neno kuntu..mi sijasumbuka na ma plug nadhani inakaribia aka mbili sasa pengine nahitaji kucheki hiyo pia..denso original unanunua wapi manake mtaani unapigwa bei za original ili hali bidhaa famba..
 
Dah niliziotea Ilala kwa ustadhi mmoja! Mwanzo nilikuwa na NGK sababu nilikuwa mkoani ambako Denso kupata ni ishu hata ukipata wanauza 35K kwa moja 😁😁😁 ila hapa dar jamaa aliniuzia 15K kila moja.
 
Nawapeni pole.
Hii yangu ni 2.4l lakini napata 13-15kmpl combined.
 
Engine ya 1ZZ inaelezwa kuwa ziko poa, kwanza kwa kuwa ni VVT-i, pili kwa kuwa ni size ya kati(cc 1800 hivi)!
Ama tukija kwenye hoja ya muanzisha uzi, hata mimi nilitaka kujua ni vitu gani hasa husababisha gari kubadili tabia na kuanza kula mafuta? Je ni:
1. Plugs
2. Nozzle
3. Gear Box kuchoka
4. Engine kuchoka
5. Uchafu kwenye air cleaner
6. Ubovu wa Throttle switches
7. Ubovu wa Oxygen Sensor switch.

Na je machine ukipima kama taa ya CHECK ENGINE haijawaka, itaweza kweli kugundua ubovu?

Kwa mdau ambae nimeona humu akiwa yuko vizuri tunaomba atupe mwanga kidogo juu ya mambo haya
 
Fika mpaka kituo cha mafuta cha Oilcom pale Magomeni Kagera, then nipigie. Ni karibu sana kutoka pale.
Ukiwa unatoka mjini ni kulia au kushoto!?
Bahati Mbaya Morogoro road huwa naikwepa sana siku hizi baada ya njia nyingi za kuvuka upande wa pili kutoingilika, hivyo najikuta nimesahau kila kitu.

Swali, kuna kile kituo jirani na njiapanda ya kuelekea Tandale Uzuri/ na Magomeni Quarter, je siyo pale? Kama ni hapo napafaham
 
ni upande wa kushoto ukiwa unatoka ubungo, unapomaliza tu kituo cha mwendo kasi cha Kagera hiyo sheli ipo mkono wa kushoto.
 
Na je machine ukipima kama taa ya CHECK ENGINE haijawaka, itaweza kweli kugundua ubovu?

Mkuu sifahamu kwa watu wengine ambao wanapima. Ila mimi mtu akiniletea gari yake akaniambia inakula mafuta huwa nakuwa na pande mbili za kupima. Ambazo ni

1. Huwa nasoma kama kuna code ya Oxygen sensor au MAF sensor au code yoyoye itakayotokea ambayo najua inaweza kuifanya gari ile mafuta.

2. Huwa naangalia live data

Hayo masuala ya codes naomba tuachane nayo maana ni mara chache sana yamekuwa na msaada. Si mashine zote zinakuwa na live data ila mashine nyingi zina hiki kitu. Hebu tuangalie hizo live Data.

LIVE DATA.

Live data huwa inaonesha performance ya components mbalimbali katika gari lako mfano sensors n.k.

Katika live Data huwa naangalia vitu vikubwa vitatu.

1. Flow rate ya hewa kwenye MAF sensor

Hii huwa haina mambo mengi, flow rate ya hewa inatakiwa kuwa kati ya 2g/s mpaka 6g/s. Ikiwa chini ya mbili au juu ya 6 basi kifuatacho ni kusafisha MAF au kununua nyingine.

2. Fuel Trims za Oxygen sensors.

Hiki ni kipengele kirefu, Lakini kwa kifupi fuel trims ni adjustments ambazo control unit ya engine huwa inazifanya ili kupata balanced Air/Fuel mixture. Kwa lugha rahisi control unit huwa inasahihisha kiasi cha mafuta kinachoingia kwenye engine. Kama control unit inapata taarifa kwamba engine inapokea mafuta machache basi itacommand injectors zikae wazi muda mrefu zaidi ili mafuta mengi zaidi yaingie kwenye engine and vice versa.

Sasa fuel trims zipo za aina mbili, Kuna Long Term Fuel Trim(LTFT) na Short Term Fuel Trim(STFT). Na huwa zinaandikwa kwa mfumo wa asilimia.

LTFT inatakiwa kuwa kati ya -10% mpaka +10%. Kama ikiwa zaidi ya +10% basi gari yako inatumia mafuta vibaya sana na ikiwa chini ya -10% gari yako inatumia mafuta kidogo kuliko kawaida (nayo ina madhara).

STFT inatakiwa kuwa kati ya -3% mpaka +3%

Sasa ukishajua kwamba gari yako inakunywa mafuta inabidi uanze kutafuta kwanini STFT na LTFT ziko nje ya range shida ni nini? Inaweza kuwa O2 sensor, kuchomoka kwa hose yoyote n.k. Nimeandika japo kwa kifupi ila maelezo ya hizi fuel trims ni marefu.

3. Oxygen sensor Voltage.

Voltage za oxygen sensor hutegemea aina ya Oxgyen sensor kama ni sensor 1 au sensor 2.

Sensor 1 ambayo hufungwa kabla ya catalytic converter(mtungi) inatakiwa kuwa na 0.1v mpaka 0.9v na huwa inafluctuate sana. Ikiwa nje ya hapo kanunue sensor nyingine.

Sensor 2 ambayo hufungwa baada ya catalytic conveter(mtungi) inatakiwa kuwa 0.5v na huwa haichezi sana.

Pia ukikuta sensor inatoa 0v huenda sensor mbovu au nyaya zake zimekatika.

Ni hayo tu.
 
Daaa, ahsante sana somo murua kabisa. Yote kwa yote nitakutafuta Mungu akipenda
 
1ZZ-FE ni kama hio ya Voltz tu, Plugs zikichoka ndio inanipa 7km/l au chini. Ila engine idle time kama kwenye foleni ndio inakula wese kuliko unavyoweza fikiri kama uko Dar ni maumivu tu.
Aisee!! Bora nimepata huu ushuhuda pia. Yangu niliwahi kuipeleka sana kwa mafundi kwa sababu nilikuwa ninaona napata 7km/l kwenye 1ZZ-FE. Mwishowe nilikuja kukata tamaa kuwa huenda ndio uwezo wa gari husika. Na kwenye foleni ukikaa mara 2-3, matokeo utayaona tu wese linavyoisha haraka.
 
Mi huwa nazima kabisa maana foleni ni maumivu 😂😂😂 kwangu nakula zangu mziki tu!
1ZZ-FE imelengwa ikupe 8KM/L economy ikiwa town trips so ikikupa 7KM sio mbaya ni sababu ya wear and tear impact plugs ama air cleaner! Ukibadili plug na cleaner au MAF sensor inaweza kurudi 8KM/L au zaidi ila highway inakula vizuri tu lazma ikupe 12KM/L
 
Mkuu sifahamu kwa watu wengine ambao wanapima. Ila mimi mtu akiniletea gari yake akaniambia inakula mafuta huwa nakuwa na pande mbili za kupima. Ambazo ni

1. Huwa nasoma kama kuna code ya Oxygen sensor au MAF sensor au code yoyoye itakayotokea ambayo najua inaweza kuifanya gari ile mafuta.

2. Huwa naangalia live data

Hayo masuala ya codes naomba tuachane nayo maana ni mara chache sana yamekuwa na msaada. Si mashine zote zinakuwa na live data ila mashine nyingi zina hiki kitu. Hebu tuangalie hizo live Data.

LIVE DATA.

Live data huwa inaonesha performance ya components mbalimbali katika gari lako mfano sensors n.k.

Katika live Data huwa naangalia vitu vikubwa vitatu.

1. Flow rate ya hewa kwenye MAF sensor

Hii huwa haina mambo mengi, flow rate ya hewa inatakiwa kuwa kati ya 2g/s mpaka 6g/s. Ikiwa chini ya mbili au juu ya 6 basi kifuatacho ni kusafisha MAF au kununua nyingine.

2. Fuel Trims za Oxygen sensors.

Hiki ni kipengele kirefu, Lakini kwa kifupi fuel trims ni adjustments ambazo control unit ya engine huwa inazifanya ili kupata balanced Air/Fuel mixture. Kwa lugha rahisi control unit huwa inasahihisha kiasi cha mafuta kinachoingia kwenye engine. Kama control unit inapata taarifa kwamba engine inapokea mafuta machache basi itacommand injectors zikae wazi muda mrefu zaidi ili mafuta mengi zaidi yaingie kwenye engine and vice versa.

Sasa fuel trims zipo za aina mbili, Kuna Long Term Fuel Trim(LTFT) na Short Term Fuel Trim(STFT). Na huwa zinaandikwa kwa mfumo wa asilimia.

LTFT inatakiwa kuwa kati ya -10% mpaka +10%. Kama ikiwa zaidi ya +10% basi gari yako inatumia mafuta vibaya sana na ikiwa chini ya -10% gari yako inatumia mafuta kidogo kuliko kawaida (nayo ina madhara).

STFT inatakiwa kuwa kati ya -3% mpaka +3%

Sasa ukishajua kwamba gari yako inakunywa mafuta inabidi uanze kutafuta kwanini STFT na LTFT ziko nje ya range shida ni nini? Inaweza kuwa O2 sensor, kuchomoka kwa hose yoyote n.k. Nimeandika japo kwa kifupi ila maelezo ya hizi fuel trims ni marefu.

3. Oxygen sensor Voltage.

Voltage za oxygen sensor hutegemea aina ya Oxgyen sensor kama ni sensor 1 au sensor 2.

Sensor 1 ambayo hufungwa kabla ya catalytic converter(mtungi) inatakiwa kuwa na 0.1v mpaka 0.9v na huwa inafluctuate sana. Ikiwa nje ya hapo kanunue sensor nyingine.

Sensor 2 ambayo hufungwa baada ya catalytic conveter(mtungi) inatakiwa kuwa 0.5v na huwa haichezi sana.

Pia ukikuta sensor inatoa 0v huenda sensor mbovu au nyaya zake zimekatika.

Ni hayo tu.
Mkuu upo vizuri, huwa unapima bei gani ili siku moja nisogee hapo unikagulie chuma changu chakavu toka ujapani 😁
 
Back
Top Bottom