Site yenyewe hii hapa:
Ni website ambayo nilijisajili na hatimaye nikawa nina-print slalary slips zangu kuanzia March 2017
- Salary slip ya kwanza niliyopata kutoka kwenye website hii ni ya March 2017
- Niliendelea kupata Salary slip hizi hadi December 2018
- Baada ya hapo, kuanzia February 2018 site ikawa inarudisha ujumbe kuwa iko kwenye matengenezo hadi leo
- Kuanzia pale sina Salary Slip hadi leo
- Nikijaribu kujisajili kule kwingine Wizara ya Fedha, Napata ujumbe kuwa Chek Namba, e-mail address pamoja na namba yangu ya simu nilivyotumia tayari vilshatumika na mtu au watu wengine
Attachment mbili zilizopo hapo chini zinaonyesha home page yake namna ilivyotokea jana tarehe 13/01/2021, lakini sikuweza ku-login, ilikuwa inaleta time-out error. Nimejaribu leo tena tarehe 14/01/2021, imeanza tena kuleta ujumbe “MFUMO HUU KWA SASA UPO KWENYE MATENGENEZO SAMAHANI KWA USUMBUFU ULIOJITOKEZA. ASANTE”. Huu ni ujumbe ambao nimekuwa nikiupokea tangu February 2018 na sina Salary Slips tena kuanzia pale hadi leo.
Je, ni kweli kwamba hii site ilikuwa genuine na ni ya Serikali?