Msaada Tutani........

Msaada Tutani........

Huwa silipi fundi kabla hajamaliza kazi, huwa sinunui vifaa kama sina uhakikika kuwa ndo vyenye hitilafu, hua simpi fundi pesa kwenda nunua vifaa mwenyewe lazima tuwe man to man, kama fault ni kubwa nachukua job mapumziko ya siku tatu kusimamia show mwenye mpaka mwisho, kama sina muda na park gari home mpaka nipate muda
Kwangu ilikuwa mgumu mkuu kufanya hivyo, ukizingatia nilikuwa namuamini. bei ya vifaa ilikuwa sawa ila kitu ambacho sikuhakikisha kama ndivyo vilikuwa vinahitajika. ila hilo ni tatizo dodgo kufahamu maana itabidi nimuombe anipe vifaa alivyotoa.
 
Huku niliko kufumuliwa marinda nikitu cha kawaida mkuu. hivyo hilo linaweza lisimtishe.
Kuwa mkali ni njia pekee ya kufanya utengenezewe gari au jamaa arudishe pesa... pesa ndefu sana hiyo mkuu wewe mteke hata muweke stoo ya mkaa siku 2 bila kula
 
Habari za asubuhi GT.

Jamani kuna fundi magari nahitaji kumpeleka police; nilisha mfahamisha kuhusu huo mpango lakini kwa jinsi anavyoongea inaonekana kama vile nitakuwa namuonea.

Ilikuwa hivi;
Gari yangu iliungua clutch nikiwa nikiwa safarini kuelekea mahali fulani. Niliipeleka kwa fundi ili awaeze kuitengeneza. kabla ya kuishusha gia box, nilimuuliza fundi makadirio ya gharama akaniambia itagharimu kama laki tatu hivi, basi nikampa go ahead. Aliomba advance ya el 50 nikampa. kwa kuwa nilikuwa na safari kesho yake nilimwambia fundi anijulishe gharama halisi za spea pale atakapokuwa ameshusha gia box.

Nikiwa safarini fundi alinipigia simu akaniambia kuwa gharama za spea zimeongezeka hadi laki 7, hivyo pamoja na ufundi itakuwa laki 9. basi nilimuambia fundi anisubiri hadi nitakaporudi. baada ya siku 3 nilirudi nakamuomba fundi aicahe gari hadi mwisho wa mwezi ukizingatia ilikuwa tare 14 ya mwezi na nilikuwa na milioni 1 tu mfukoni, hivyo sikuona umuhimu wa kutengeneza gari alafu niishie kuteseka wiki mbili mpaka pale nitakapata mshahara.

Fundi alikubali na akanishauri gari tuite garage tuipaki sehemu salama kuepuka kuibiwa vifaa.
gari ilihamishwa na kupelekwa sehemu ya lulipia.

Ilipofika tu mwisho wa mwezi nilimpelekea fundi pesa zote za spea, oil na nikamlipa pesa zote za ufundi. toka nimlipe pesa alianza kunizungukusha kuwa kuna gari alikuwa ameshusha ingine hivyo imemsumbua kiasi kwamba hakuweza kushughulikia gari yako. ilikuwa siku ya jumatano akaniahidi kutengeneza yangu jumamosi.

Ilipofika jumamosi nilimpigia simu kumuuliza kama anaendelea na matengenezo ya gari yangu, akasema kuwa alikuwa msibani akitoka ataenda kuichukua tulipo ipaki. ilipofika jioni akanipigia simu kuwa ufunguo wa gari umepotea hivyo nimpe spea kama ninayo; nika mwambia sina spea.

baada ya kumwambia kuwa sina spea akasema watengeneza ufungu wa kuchonga, nikamwambia kuwa gai haitumi funguo za kuchonga, yeye akaniambia nisiwe na wasiwasi. ilimaliza zaidi ya wiki kila nkimpigia simu anasingizia kuwa bado wanatafuta suluhisho la funguo.

Jumatatu iliyopita nilikwenda gareage nikakuta wanamalizia kufunga ingini. baada ya siku kama tatu kilia nikimpigia fundi ananiambia kuna sensa ziliibiwa hivyo anatafuta za kuliplace. ilitakiwa nichukue gari ijumma (jana) nilipompigia akaniambia gari bado kaipeleka kwa fundi wiring. tena alikuwa ananijibu hovyo.

jamani mtu kama huyu nimfanyeje ? ukizingatia licha ya kumlipa ananizungusha kwa mda wa wiki tatu sasa jambo ambalo linaniongezea hasara kwani natakiwa kukodi tax kwa wiki mara tatu kwa ajili ya shughuli ninanzo zifanya ambazo ziko kama kilometre 40 toka nilipo (yaani 80 kwenda na kurudi)

aasnteni

Pole mkuu.

Ushauri wangu kwa ajili ya siku nyingine.Ukiwa na kazi yoyote ile usimlipe fundi hela yote hadi akukabidhi kazi iliyoisha.Hata akikuomba advance ukiweza umpe advance pungufu ya aliyokuomba.Mafundi wengi wakishachukua hela hawafanyi kazi.
 
Pole mkuu.

Ushauri wangu kwa ajili ya siku nyingine.Ukiwa na kazi yoyote ile usimlipe fundi hela yote hadi akukabidhi kazi iliyoisha.Hata akikuomba advance ukiweza umpe advance pungufu ya aliyokuomba.Mafundi wengi wakishachukua hela hawafanyi kazi.
nimejifunza kitu hapa
 
NDIO UJIFUNZE KUPELEKA GARI KARAKANA AMBAZO ZINAAMINIKA NA SIO HAWA FUNDI UCHWARA WA KUUNGA UNGA MTAANI

MCHUKULIE HATUA ZA KISHERIA NA FIDIA AKULIPE
 
NDIO UJIFUNZE KUPELEKA GARI KARAKANA AMBAZO ZINAAMINIKA NA SIO HAWA FUNDI UCHWARA WA KUUNGA UNGA MTAANI

MCHUKULIE HATUA ZA KISHERIA NA FIDIA AKULIPE
Nikisha wahi kuoeleka karakana moja tena ni dealer wa Toyota. Sitakaa nirudie tena.
Ameileta lakini baada ya kumfikisha police
 
Back
Top Bottom