Msaada: TV Hisense Inch 55 imeacha kuonyesha picha

maramojatu

JF-Expert Member
Joined
Mar 16, 2012
Posts
1,749
Reaction score
2,319
WanaJF,

Poleni na majukumu.
Kama mada inavyosomeka kwenye kichwa cha habari TV ya Hisense imeacha kuonyesha picha na ninahisi kwamba kama bulb zake zimeungua.

Msaada tafadhali kwa mafundi waliopo kwenye group ili niweze kuitumia bila gharama kubwa.

Asante,

Maramojatu
 
Tafuta fundi mzuri
 
Mimi yangu imebutuka kama kamlipuko ikazima sijasumbuka nayo hata kujua shida nini nna matatizo mengi nimeona niiache mpaka ntakapokuwa sawa au ining'inie hapo forever
Hope matatizo yataisha muda si mrefu na utatafuta fundi airekebishe. Pole sana
 
Ohh Hisense tena,,, hizo kwa sasa kuotea kupata og ni kwa mbinde,, mjini zimejaa feki na zinasumbua sana ninalo langu nimeliweka tu kwenye box nalo shida kioo ni ya inch 58 au 60 hivi
Yangu nahisi ni OG... Niliinunua Zenji na jamaa wakanihakikishia kuwa ni yenyewe
 
Adapter unayoitumia inaendana na tv? kwa maana ya voltage. Kuna scenario mtu ananunua TV mpya kisha anatumia adapter ya zamani ambayo unakuta ni ndogo kiutendaji. Ni kama kununua simu janja (kubwa) halafu unaichaji kwa kutumia charger ya simu kitochi (ndogo)
 
Vyote ninavyotumia vilikuwa part of the package.
 
Ohh Hisense tena,,, hizo kwa sasa kuotea kupata og ni kwa mbinde,, mjini zimejaa feki na zinasumbua sana ninalo langu nimeliweka tu kwenye box nalo shida kioo ni ya inch 58 au 60 hivi
mi Nina mpango wa kununua 55nch nataka niende posta Kwa authorized dealer vip unanishaur vipi maana waliniambia 1:1m
 
point kubwa sana hii
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…