Msaada TV ya LG

Han Solo

JF-Expert Member
Joined
Jan 2, 2020
Posts
461
Reaction score
1,075
Siku za nyuma nilinunua Smart TV ya LG yenye ukubwa wa inch 55 model number 55SM90. Katika Katika kui unbox nikabandua karatasi la plastiki lililokuwa kwenye kioo nikidhani ni yale makaratasi kama kwenye simu kumbe ni sehemu ya kioo, nimeshtuka nimeshabandua mpaka katikati nikawasha TV nusu haiwaki sehemu niliyo bandua.

Nikaenda Mnazi mmoja kwenye workshop ya LG, muhindi akaniambia kubadili kioo inabidi nitoe 1.5m kiagizwe korea na kitafika baada ya miezi mitatu, nikaona heri ninunue TV ingine.

Shida ni hii iliyoharibika nimekaa nayo muda mrefu iko ndani tu.

Hakuna namna naweza iuza? au kupata kioo replacement cha bei nafuu?

Dah pole sana.

Walipaswa waandike maelekezo.
 
Ungesoma maelekezo yasingekukuta hayo, weka kumbukumbu ya kuacha kudhani.
 
Katika kui unbox nikabandua karatasi la plastiki lililokuwa kwenye kioo nikidhani ni yale makaratasi kama kwenye simu kumbe ni sehemu ya kioo, nimeshtuka nimeshabandua mpaka katikati nikawasha TV nusu haiwaki sehemu niliyo bandua.
Kwamba ni rahisi hivyo kubandua plastic. Pole sana mkuu, sema LG utaishi nayo sana kwa ubora ule ule.
 
me hiyo tv ninayo hapa sema shida yake inatoa mistali kwenye kioo pembeni nimtumia miaka mwili tu imeanza iyo shida. bali sema ina vitu vingi hata watu wangukani pia walikuwa hajui ivyo vitu
 
Ushauri wangu ni kwamba rudi dukani ulipoinunua, huenda muuzaji akawa na Tv nyingine aina kama hiyo yenye tatizo jingine na kioo ni kizima ili uinunue kwa discount na kubadili kioo chake na kuhamishia kwenye yako. Wakuu nawashauri muhamie Samsung ndio mpango mzima kwenye mambo mengi ya Electronics na pia kwenye Tech ya nano Cell wako vizuri.
 
nilirudi dukani immediately kuuliza kama kuna namna wanaweza kunisaidia ila wakasema wao hawana msaada wanauza tu bidhaa mpya, wakanielekeza niende kwenye workshop ya LG mnazi mmoja, ndiyo nikaishia kuambiwa nitoe 1.5m ili waagize kioo kipya
 
Kwamba ni rahisi hivyo kubandua plastic. Pole sana mkuu, sema LG utaishi nayo sana kwa ubora ule ule.
mwanzo ilikuwa rahisi kubandua ila nilipofika katikati ikawa ngumu ndiyo nikashtuka isije ikawa naharibu, nikasema ngoja kwanza niiwashe asalaleeee ndiyo nikakutana na balaa hilo
 
mwanzo ilikuwa rahisi kubandua ila nilipofika katikati ikawa ngumu ndiyo nikashtuka isije ikawa naharibu, nikasema ngoja kwanza niiwashe asalaleeee ndiyo nikakutana na balaa hilo
Pole sana mkuu
 
Ingia mwenyewe mtandaoni labda unaweza kuipata cheaper hiyo screen ila daima kuna risk. Au uzunguke kwa mafundi ukute mwenye nayo device kama hiyo iliyokufa kitu kingine au uza for parts.
 
Sikuzote TV nikioo kikiharibika kioo niheri ugawe tu hata bure au uuze kwa hasara hivi vioo vingi vya kununua sio og na unaweza kufunga miezi michache tu vikatoa mistari tena so heri ununue new tu
 
mwanzo ilikuwa rahisi kubandua ila nilipofika katikati ikawa ngumu ndiyo nikashtuka isije ikawa naharibu, nikasema ngoja kwanza niiwashe asalaleeee ndiyo nikakutana na balaa hilo
Pole sana.
 
nilirudi dukani immediately kuuliza kama kuna namna wanaweza kunisaidia ila wakasema wao hawana msaada wanauza tu bidhaa mpya, wakanielekeza niende kwenye workshop ya LG mnazi mmoja, ndiyo nikaishia kuambiwa nitoe 1.5m ili waagize kioo kipya
Unajua hawa Maagent wa hizi kampuni zinazotuuzia vifaa vya electronics muda mwingine huwa kama wagonjwa, Tv mpya 2/2.5m, ila kioo ni 1.5m si ni bora ujipange ununue nyingine mpya. Hamia Samsung mkuu. Lakini pia usikate tamaa endelea kutafuta utafanikiwa.
 
nilirudi dukani immediately kuuliza kama kuna namna wanaweza kunisaidia ila wakasema wao hawana msaada wanauza tu bidhaa mpya, wakanielekeza niende kwenye workshop ya LG mnazi mmoja, ndiyo nikaishia kuambiwa nitoe 1.5m ili waagize kioo kipya
Ngoja kwanza kitu ulichobandua kinafananaje? kama karatasi flani hivi tinted au?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…