Msaada: Typhoid inanitesa sana...

Msaada: Typhoid inanitesa sana...

Lavit

JF-Expert Member
Joined
May 16, 2011
Posts
14,834
Reaction score
32,522
Wakuu ni muda mrefu sasa toka nianze kusumbuliwa na huu ugonjwa, kwa kifupi sijawahi pona mpaka nikawa fit kabisa! Mwili wangu umekuwa na uchovu kila muda hata kazi zangu haziendi kwa ufanisi.

Nimetumia dawa nyingi sana, za hospital mpaka za kienyeji lakini wapi! Hapa nilipo nina kama wiki toka nimalize dozi ila hali ni mbaya vile vile.

Imefika muda nakata tamaa, haiwezekani kila siku niumwe mimi tu! Kama ni kanuni za afya nafuata, maji ya kunywa nanunua, ya kuoga naweka waterguard, hata kula najitahidi kula sehemu zenye mazingira masafi!

Pengine humu kuna watu wamewahi pitia hali kama hii, je mlitumia tiba gani? Na kwa madaktari naomba recommendation ya dawa ambazo zinaweza zikanipa tiba ya kudumu!

Natanguliza shukrani!!
 
Pole sana mkuu...ila una uhakika kabisa kuwa ni typhoid? Umepima wapi na kwa muda mrefu umekuwa ukitumia dawa gani?...ushawahi kufanya culture ili utibiwe kwa dawa maalumu?
 
Pole sana mkuu...ila una uhakika kabisa kuwa ni typhoid? Umepima wapi na kwa muda mrefu umekuwa ukitumia dawa gani?...ushawahi kufanya culture ili utibiwe kwa dawa maalumu?
Asante mkuu...nimefanya vipimo vingi vingine sikumbuki, ila last time nimeenda Agha khani, bado wakakuta typhoid...culture nilifanya muda mrefu nadhan ni 2012 hakukuwa na shida yeyote!

Baadaye nikisoma jina la dawa nitaweka hapa!
 
Ni nini basi? Ebu niambie naweza fanya vipimo gani vya ziada
umeambiwa hapo juu fanya stool culture, isipoleta majibu ni typhoid basi ni ugonjwa mwingine kabisa.
Halafu usisahau kipima na HIV maana daaaaah
 
Tatizo hilo laweza kuwa ni hili lililogunduliwa cku za karibuni, linahusu BACTERIA ila sio wale wa Typhoid but ni bacteria walio mwilini mwako kwa kazi maalum ya uyeyushaji wa chakula (Flora). Imegundulika kuwa bacteria hawa muhimu na wasio na madhara waweza geuka na kuwa wabaya pale panapotokea changes kwenye GIT yako hasa kwa kusababishwa na Stress, Alcohol, etc. Tatizo hili kwa kitaalamu linaitwa Small Intestine Bacterial Overgrowth (SIBO), check for that!
 
Back
Top Bottom