Msaada:: Typhoid inanitesa!!

Msaada:: Typhoid inanitesa!!

tindikalikali

JF-Expert Member
Joined
Jan 14, 2011
Posts
4,854
Reaction score
1,129
Wadau habar zenu!!

Toka huu mwaka umeanza nimekuwa nikisumbuliwa na typhoid mara kwa mara, nimetumia dawa aina tofauti tofauti mara chache napona na inajirudia tena pamoja na kufuata kanuni zote za usafi!

Mara ya mwisho nimepima wiki mbili zilizopita na nikikutwa nayo, nikapewa cipro ninywe kwa siku kumi, dozi nimemaliza Jumapili lakini hakuna mabadiliko yeyote, leo nimepima nimekutwa tena na hao wadudu wa typhoid!

Wadau naomba mwenye kujua tiba sahihi na ya kudumu kwa huu ugonjwa!

Natanguliza shukrani!!
 
Wewe unatatizo kama langu. Tunaomba waugwana watusaidie
 
Mim sio daktar bt nishawah kuwa na tatizo km hilo ila nilikuwa nakunywa sana maji so unywe sana maji
 
Kuna dawa ya asili niliwahi kuitumia na ikanisaidia na kwabahati nzuri alienitengenezea alikuwa ni baba yangu mzazi na akanifundisha jinsi ya kuianda kwakutumia miti shamba.Nimeshawatengenezea baadhi ya watu na ikawasaidia.
 
Wadau habar zenu!!

Toka huu mwaka umeanza nimekuwa nikisumbuliwa na typhoid mara kwa mara, nimetumia dawa aina tofauti tofauti mara chache napona na inajirudia tena pamoja na kufuata kanuni zote za usafi!

Mara ya mwisho nimepima wiki mbili zilizopita na nikikutwa nayo, nikapewa cipro ninywe kwa siku kumi, dozi nimemaliza Jumapili lakini hakuna mabadiliko yeyote, leo nimepima nimekutwa tena na hao wadudu wa typhoid!

Wadau naomba mwenye kujua tiba sahihi na ya kudumu kwa huu ugonjwa!

Natanguliza shukrani!!
hapo mkuu kuna ishu mbili. kwanza pengine dawa zinadunda cipro sikuhizi inadunda kwenye kutibu typhoid jaribu azithromycin. pili kuna watu wanakuwa ni chronic carriers. watu hawa huwa na wadudu wa typhoid mwililini mwao hasa kwenye mfuko wa nyongo. watu hawa mara nyingi huwa hawana dalili za ugonjwa ila huweza kusambazia wengine. sasa fikiria chronic carrier awe ni mke wako au mamantilie unakokulaga!?.

chakufanya. badilisha sehemu unayonunuaga misosi, badili dawa tumia azithro, pia wote nyumbani mkapime pengine kuna chronic carrier (mbeba vijidudu sugu).
 
Back
Top Bottom