Nina watu wawili nawafahamu, tunaishi nao Dar wote walinunua magari hayo ndani ya kipindi karibia sawa (2015) mmoja Spacio Nyeusi na Raum Blue mpauko, (wote sio old model ni hizi 2006/8) na waliagiza nje.
Hadi tunavyoongea wote still wanazo. Spacio bado inavutia kwa nje, body bado inadai.
Raum mlango ule wa kuslide umekufa, pia body yake naona kama imelegea legea maungio ya sehemu moja na nyingine yametanuka sana.
Sijui ni utunzaji au barabara ila kweli ulivosema kwenye issue ya body Spacio anajitahidi zaidi ya Raum. Nisichopenda kwa Spacio ni size ndefu sana.