kwa hizo sheria za kiislam aisee ni pagumu hata mkae miaka 20 hamgawani unapewa kiasi chochote chakuanzia maisha alichonacho mwanaume wakati huo!
hivyo wanawake wa kiislam ishini na waume zenu kwa mujibu wa dini hata kama una kipato maana ukijifanya kuchangia maendeleo nusu kwa nusu salama yako ndoa isivunjike , ikivunjika huna chako.
ila quran imeeleza mwanaume ni wajibu wake kukuvisha,kukulisha & mahitaji mengine. ( ni lazima sio hiari) ukijitia kujenga naye unalo maana hata mahakaman utaulizwa juu ya sheria za dini