Msaada: Ugonjwa wa akili

Msaada: Ugonjwa wa akili

Mbwa kala mbwaa

JF-Expert Member
Joined
Apr 16, 2013
Posts
218
Reaction score
389
Wakuu madaktari wa Jf,nina ndugu yangu mwaka jana mwezi wa nne alipatwa na matatizo ya akili,na kuanza kuongea maneno yasiyo eleweka,kudai anasikia sauti za aina mbalimbali ambazo wengine hatuzisikii,kupiga kelele ovyo na hata kujaribu kudhuru wengine na kujidhuru.

Tulimwahisha Hospitali ya Muhimbili,na alilazwa kwa wiki 2. Katika diagnosis,madaktari walisema ana "Bipolar Mania",na amekuwa akitumia dawa aina ya "Carbamazepine" na "Haloperidol" toka april mwaka jana. Hali yake sasa imekuwa stable.

Sasa nilikuwa nataka kujua: 1/Je,madawa haya ya akili kuna mwisho wa kutumia,au ni Lifetime dosage? 2/Ugonjwa huu wa Bipolar Mania unaweza kupona moja kwa moja au hauponi? AHSANTENI.
 
huyo ameshapata kilema,hawezi kuishi bila dawa naa anavyozidi kutumia kwa muda mrefu zaidi ya miaka 10 itampa shida
 
pole sana ndugu yangu,kuna ndugu yangu ana tumia hizo dawa alianza kutumia dawa hizo wakati nikiwa darasa la tatu au la pili hadi leo nimeajiliwa anaendelea kutumia kila siku,kama atakuwa huyo ndugu yako sio mvivu wa kunywa dawa mtaishinae vizuri na mtasahau swala la ugonjwa.
 
Back
Top Bottom