Msaada ugonjwa wa Figo

Msaada ugonjwa wa Figo

GedsellianTz

JF-Expert Member
Joined
Jul 5, 2016
Posts
1,348
Reaction score
1,805
Habarini wakuu.

Tumaini langu wote ni wazima. Kuna jamaa angu anasumbuliwa na figo...amekuwa akivimba mwili mara kwa mara, hospitali alichek akaambiwa ana tatizo la figo lakini hakupewa dawa zaidi aliambiwa anywe maji mengi tu, kwa sasa hali inazidi kubadilika kwani anaweza kumaliza hata siku tatu hajaenda haja, pia akaifanikiwa kwenda anapata maumivu makali sehemu ya haja kubwa.

Msaada kama kuna mtu humu anafahamu dawa anisaidie plllz. Natanguliza shukrani zangu.
 
Poleni sana mkuu.

Wajuzi watakuja watakusaidia. Poleni sana.
 
Habarini wakuu.

Tumaini langu wote ni wazima. Kuna jamaa angu anasumbuliwa na figo...amekuwa akivimba mwili mara kwa mara, hospitali alichek akaambiwa ana tatizo la figo lakini hakupewa dawa zaidi aliambiwa anywe maji mengi tu, kwa sasa hali inazidi kubadilika kwani anaweza kumaliza hata siku tatu hajaenda haja, pia akaifanikiwa kwenda anapata maumivu makali sehemu ya haja kubwa.

Msaada kama kuna mtu humu anafahamu dawa anisaidie plllz. Natanguliza shukrani zangu.
Pole sana mkuu
 
Ugonjwa wa figo siku hizi ni kama wimbo. Sijui ni kwanini. Labda ni haya maji ya chupa tunayokunywa siku hizi ila watu wengi wanaumwa magonjwa ya figo.

Watu huwa wanakosea sana wanapoumwa. Ukiumwa figo nenda kwa Daktari bingwa wa magonjwa ya figo. Ukiumwa jino nenda kwa Daktari bingwa wa Meno.

Usije ukaenda hospitali ukaonana na daktari wa kawaida ambaye siye specialist wa ugonjwa unao umwa. Kama hajaomba msaada kwa madaktari bingwa basi atakupotezea muda wakati huo ugonjwa unazidi kukomaa.
 
Sasa hapo kuna mawili hilo la figo na kupata choo kwa tabu, ushauri kama aliambiwa ana tatizo la figo moja kuna tofauti ya stage ama ukubwa wa tatizo la figo hivo ni muhimu kwenda hospi aonane na dr wa figo hospital kama regency, muhimbili, ama agha khan na kwingineko, kisha atashauriwa ni kweli imefikia hatua gani na kipi kifanyike kumsaidia kuhusu figo pia apimwe kama hana tatizo la kisukari au Presha yake kama pia huwa ni ya kawaida au ipo juu wakati wote hivo viwili vyaweza kuwa chanzo cha figo kipata tatizo japo kuna mengine pia... hilo la choo ni tatizo lingine anaweza tumia Lactulose syrup kuanzia 10mls hadi 20mls kila baada ya saa kumi na mbili, akipata choo aache kuitumia hata kama itakua baada ya kuinywa mara moja tu. Akifika hospital alieleze na hilo.

Sent from my SM-N910L using JamiiForums mobile app
 
Nashukuru mkuu, hiyo syrup ashatumia akapona kwa mda but nw hali imerudi tena
 
Habarini wakuu.

Tumaini langu wote ni wazima. Kuna jamaa angu anasumbuliwa na figo...amekuwa akivimba mwili mara kwa mara, hospitali alichek akaambiwa ana tatizo la figo lakini hakupewa dawa zaidi aliambiwa anywe maji mengi tu, kwa sasa hali inazidi kubadilika kwani anaweza kumaliza hata siku tatu hajaenda haja, pia akaifanikiwa kwenda anapata maumivu makali sehemu ya haja kubwa.

Msaada kama kuna mtu humu anafahamu dawa anisaidie plllz. Natanguliza shukrani zangu.

Pole sana Mkuu, kwanza huyo jamaa yako aanze kutafuta BIMA ya Afya (NHIF) kama hana.

Kama anayo ni hatua nzuri..... Kwani hatua zake za matibabu ni ghali sana.

Pili tiba ya Figo ni kuwekewa Figo nyingine.

Kabla ya kuwekewa Figo nyingine (mara nyingi hufanyika India kwa wagonjwa wetu wa Tanzania) Kuna vipimo lazima upitie na ni lazima upate mchangiaji wa hiyo Figo (donor).

Ukijihakikishia hayo hapo juu basi matibabu hulenga kwenye kutibu dalili zitakazojitokeza kama vile Electrolytes imbalance, uremic syndrome, anemia nk.

Pole sana, hilo ni tatizo haswaaa.
 
Wahi hospitakini wanafanya vipimo waone shida iko wapi. Kama ni kusafisha ( dialysis) basi itafanyika. Kama dawa watakupa.
 
Nashukuruni, kesho tutaenda hospital ntawapa mrejesho
 
Habarini wakuu.

Tumaini langu wote ni wazima. Kuna jamaa angu anasumbuliwa na figo...amekuwa akivimba mwili mara kwa mara, hospitali alichek akaambiwa ana tatizo la figo lakini hakupewa dawa zaidi aliambiwa anywe maji mengi tu, kwa sasa hali inazidi kubadilika kwani anaweza kumaliza hata siku tatu hajaenda haja, pia akaifanikiwa kwenda anapata maumivu makali sehemu ya haja kubwa.

Msaada kama kuna mtu humu anafahamu dawa anisaidie plllz. Natanguliza shukrani zangu.
Mkuu pole sana kwa matatizo ya ndugu yako nitafute mimi nipate kumtibia hilo figo lake apate kupona. Ukihitaji matibabu toka kwangu unaweza kunitafuta kwa Mawasiliano MziziMkavu Email barua ya pepe. fewgoodman@hotmail.com What's App na Viber +905344508169
 
Back
Top Bottom