Kuna kiumbe kinanyonya RBC zake nini sio upungufu wa Madini chuma kweli?
Sababu za upungufu wa damu mwilini:-
1. Upungufu wa madini ya chuma mwilini
2. Upungufu wa vitamini A na B-12 mwilini
3. Maradhi kama HIV, UKIMWI, saratani, mardhi ya figo haya huweza kuleta upungufu wa damu
4. Mfumo wa kinga mwilini kuuwa na kuharibu seli hai nyekundu (autoimmune)
5. Uharibifu wa seli hai nyekundu kufanyika kwa haraka kuliko utengenezwaji.
6. Kuwa na maradhi ya sickle cell anemia
Kazi za damu mwilini:-
1. Kusafirisha viinilishe kutoka katika mfumo wa mmeng’enyo wa chakula kwenda maeneo mbalimbali ya mwili.
2. Kusafirisha hewa ya oksijeni kutoka kwenye mapafu kwenda maeneo mengine ya mwli.
3. Kusafirisha hewa ya kabonikaiyoksaidi kutoka kwenye seli na kupeleka kwenye mapafu kwa ajili ya kutolewa nje
4. Kudhibiti joto la mwili kwa kulipooza inapohitajika na kuliongeza inapohitajika
5. Kusafirisha homoni kwenda maeneo mbalimbali ya mwili.
Vyakula vya kuongeza damu mwilini:-
1.Nyama nyekundu kama nyama ya ng’ombe, mbuzi na Kondoo
2.Maini
3.Nyama ya figo
4.Mboga za rangi ya kijani kama mchicha na spinachi
5.Maharagwe
6.Kunde
7.Mayai
8.Nafaka nyinginezo
9.Njegere
10.Korosho na karanga
11.Samaki
12.Nyama ya ndege
13.Karoti
14.Matikiti
15.Zabibu
16.Viazi vitamu
17.Matunda yenye uchachu kama machungwa, ndimu na limao.
18.Polipili nyekundu