Msaada: Ugonjwa wa mbuzi kuzunguka. Huu ni ugonjwa gani?

Msaada: Ugonjwa wa mbuzi kuzunguka. Huu ni ugonjwa gani?

Leodigardcyrilo said:
dhibiti kupe wape antibiotics
Asante mkuu. Ntajitahidi kupambana na kupe, kuhusu antibiotics huwa nawapa ila ni patupu mkuu.
 
Jamani kunamtu hapa alisema alikwenda SUA akapata baadhi ya maelezo sasa tulimwomba atumegee kidogo lakini kimyaaa wengi humu niwafugaji hata kama sio kwa biashara, ingetusaidia elimu juu ya hili.
 
Habarini!

Mbuzi wangu wamekuwa wakisumbuliwa na ugonjwa wa kuzunguka. Yaani huu ugonjwa mbuzi akiugua anashindwa hata kutembea (anabaki kuzunguka tu hapo hapo) na unaonekana huwa unaathiri upande fulani wa mbuzi.

Kwa mfano, akiathirika sana kiasi cha kushindwa kusimama, yaani akishalalia tu upande wa kushoto basi hawezi kulalia upande wa kulia hata kama unamgeuza.

Yaani ukimgeuzia huo upande mwingine utakuta anajigeuza haraka sana (inakuwa mithili ya ncha za sumaku ambazo haziendani).

Naomba msaada wa namna yoyote wa tiba, chanjo na jina la ugonjwa kitaalamu.
Ndugu upo Dar?
 
ivi dj ajapiga kizunguzungu maeneo ayo,isijekuwa mbuz wanaelewa wimbo..
Habarini!

Mbuzi wangu wamekuwa wakisumbuliwa na ugonjwa wa kuzunguka. Yaani huu ugonjwa mbuzi akiugua anashindwa hata kutembea (anabaki kuzunguka tu hapo hapo) na unaonekana huwa unaathiri upande fulani wa mbuzi.

Kwa mfano, akiathirika sana kiasi cha kushindwa kusimama, yaani akishalalia tu upande wa kushoto basi hawezi kulalia upande wa kulia hata kama unamgeuza.

Yaani ukimgeuzia huo upande mwingine utakuta anajigeuza haraka sana (inakuwa mithili ya ncha za sumaku ambazo haziendani).

Naomba msaada wa namna yoyote wa tiba, chanjo na jina la ugonjwa kitaalamu.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kupona inakuwa ngumu sana kwa sababu moyo unakuwa na maji na pia kuna kuwa uvimbe kwenye tezi,kwaiyo unapotumia tetracycline pekee utatibu vidudu tu vya ugonjwa lakn kuna maji kwenye moyo na hayo mauvimbe unakuwa umeyaacha na ndio yanayomuua mnyama.....kinga ni kuwaogesha tu ili kuua kupe coz ndio causative agent... Kupe anamagonjwa mengi sana kwa mnyama na yote ni hatari sana cha muhimu mtafute Dr naamini utapata ushauri mzuri na mengne mengi katika ufugaji wako mkuu.

Sent using Jamii Forums mobile app
Wataalamu wengine tabu sana, unawezaje kutumia dalili moja kuconclude kwamba ugonjwa ni cowdriosis? una uhakika hao mbuzi wako na Amblyomma ticks infestations?

Yako magonjwa mengi yenye dalili za kuzunguka na sio cowdriosis pekee, kwa nini hujaelezea uwezekano wa kuwa huenda ni hayo? au hujui kama mnyama akipata bacterial meningitis pia huzunguka? what about encephalitis?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
huo ni heart water disease akianza hvyo ujue kupona ni mara chache kaka

Sent using Jamii Forums mobile app
Sio lazima iwe heart water msikariri, mala nyingi kwa mbuzi na kondoo huwa ni Listeriosis, ugonjwa huu husababishwa na bacteria wanaoitwa Listeria monocytogenes, signs na symptoms nyingi ni kama za cowdriosis lakini kwa Listeriosis mzunguko wake ni wa upande mmoja pekee, kwenye heart water lazima mnyama atoe povu mdomoni wakati kwa Listeriosis hudondosha mate upande mmoja sababu ya partial paralysis.

Listeriosis pia prognosis yake ni issue though ukiiwahi mala chache wanyama hurecover, Listeriosis ndo husababisha Encephalitis so sometimes wengi huita tu encephalitis though sio sawa.

Ndugu yangu haya majibu yako yapo kitaalamu zaidi, ungetumia lugha laini kuelezea maana sio wote ni madaktari kama wewe. Sisi wengine ni wakulima tu, na tungependa kupata majibu murua tuwaponye hawa mbuzi wetu, ubaya wake sasa hayo majibu yanazidi kutuongezea kizunguzungu na sisi pia 😀😀😀
 
Sasa atatokaje na mbuzi huko katerero au rubondo hadi Sua...!?
Akimpakisha kwenye bus abiria wakianza kuzunguka huko ndani itakuwaje...!

Sent from my iPhone using JamiiForums
hahahah
 
Sumve 2015 said:
Tofauti na kuzunguka wako na dalili zipi nyingine?
Mkuu dalili znazoonekana sana ni;
~Mbuzi huanza kuzubaa,
~Kuanza kulia (kupiga kelele) mithili ya anayepata maumivu fulani.
~Baadae huanza kutokwa na maji maji mdomoni.
 
Mkuu dalili znazoonekana sana ni;
~Mbuzi huanza kuzubaa,
~Kuanza kulia (kupiga kelele) mithili ya anayepata maumivu fulani.
~Baadae huanza kutokwa na maji maji mdomoni.
Mkuu kwanza pole kwa kupatwa na hali kama hiyo kwenye mifugo yako.
Mimi nitatoa maelezo kiasi ambayo yatakusaidia,
Kwanza Mbuzi,Kondoo na Ng'ombe ni baadhi ya Wanyama ambao tumbo Lao limegawanyika katika sehemu nne (Ruminants), kwa kawaida wanyama hawa hushambuliwa sana na magonjwa ambayo vimelea (wadudu) wake husambazwa na kupe ambapo vimelea hivyo huweza kusababisha magonjwa kwa wanyama.

Baadhi ya magonjwa hayo ni;
•Anaplasmosis (Ndigana baridi)
•ECF (Ndigana Kali)
•Heartwater (Maji kwenye moyo/kuzungukazunguka)
•Babesiosis ( Mkojo mwekundu)
•n.k
Njia bora za kuwakinga mifugo wako na magonjwa tajwa hapo juu ni;
1. Kutumia njia bora za ufagaji (good management)
2. Kuwapa chanjo za magonjwa husika
3. Kuosha mifugo yako angalau mara 1 au 2 kwa wiki ili kuangamiza Kupe.

Twende kwenye mada uliyoleta;
•Inaonesha kabisa Mbuzi wako wameathirika katika mfumo wa fahamu (Nervous system).

•Kutokana na historia uliyotoa ya Mbuzi wako ni ngumu kwa hapa kutaja ugonjwa moja kwa moja ni upi ila nitataja baadhi ya hali/magonjwa ambayo yanahusisha dalili zinazofanana na hizo:
1. Rabies ( Kichaa cha mbwa)
2. Heartwater (maji kwenye moyo)
3. Listeriosis/circles (ugonjwa wa kuzunguka)
4. Encephalitis ( sina kiswahili chake)
5. Meningitis
6. Cerebral babesiosis
7. Cerebral ECF
8. Sumu aina ya Strychnine
.................
1. Rabies husababishwa na virusi(Lyssa virus) ni ugonjwa hatari wa kichaa cha mbwa huwapata sana mbwa lakini unaweza wapata pia paka,mbuzi,ng'ombe,kondoo na binadamu. Ugonjwa huu husambaa kwa ama kung'atwa na mbwa mwenye ugonjwa tajwa au mate ya mbwa aliyeathirika kugusa kwenye kidonda au sehemu za wazi za mwili za mnyama, kuzungukazunguka ni moja ya dalili ya Rabies.
2. Heartwater husababishwa na "Cowdria ruminantium" ni ugonjwa ambao husababisha maji kwenye moyo vijidudu hushambulia seli za mishipa ya damu nakupelekea kufuja kwa maji maji hatimae maji kujaa kwenye kuta za moyo, vijijidudu hivi hushambulia hadi mishipa ya kichwani (ubongo) na kupelekea dalili ya kuzungukazunguka.
3.Listeriosis ni ugonjwa unaosababishwa na bacteria aina nyingi ambao hushambulia seli za ubongo na kupelekea meningitis au encephalitis ambazo huleta dalili ya kuzungukazunguka.
4. Cerebral ECF, Cerebral babesiosis na sumu ya Strychnine huathiri mfumo wa ufahamu na kusababisha hali kama ya degedege na kuzungukazunguka.

Mimi pia siko mbali sana na wachangiaji wengine napendekeza magonjwa mawili kati ya yote hapo juu;
1. HeartWater (maji katika moyo) na
2. Listeriosis/ circles (kuzunguka)
Magonjwa haya hutibiwa kwa kutumia Antibiotics endapo yatagundulika mapema ila ukichukua muda ni ngumu kutibika.

Nakushauri utafute mtaalamu wa mifugo aliyekaribu na wewe akusaidie, matumizi ya ovyo ya Antibiotics, pasipo utaalamu huleta usugu wa magonjwa.
 
Back
Top Bottom