Mkuu dalili znazoonekana sana ni;
~Mbuzi huanza kuzubaa,
~Kuanza kulia (kupiga kelele) mithili ya anayepata maumivu fulani.
~Baadae huanza kutokwa na maji maji mdomoni.
Mkuu kwanza pole kwa kupatwa na hali kama hiyo kwenye mifugo yako.
Mimi nitatoa maelezo kiasi ambayo yatakusaidia,
Kwanza Mbuzi,Kondoo na Ng'ombe ni baadhi ya Wanyama ambao tumbo Lao limegawanyika katika sehemu nne (Ruminants), kwa kawaida wanyama hawa hushambuliwa sana na magonjwa ambayo vimelea (wadudu) wake husambazwa na kupe ambapo vimelea hivyo huweza kusababisha magonjwa kwa wanyama.
Baadhi ya magonjwa hayo ni;
•Anaplasmosis (Ndigana baridi)
•ECF (Ndigana Kali)
•Heartwater (Maji kwenye moyo/kuzungukazunguka)
•Babesiosis ( Mkojo mwekundu)
•n.k
Njia bora za kuwakinga mifugo wako na magonjwa tajwa hapo juu ni;
1. Kutumia njia bora za ufagaji (good management)
2. Kuwapa chanjo za magonjwa husika
3. Kuosha mifugo yako angalau mara 1 au 2 kwa wiki ili kuangamiza Kupe.
Twende kwenye mada uliyoleta;
•Inaonesha kabisa Mbuzi wako wameathirika katika mfumo wa fahamu (Nervous system).
•Kutokana na historia uliyotoa ya Mbuzi wako ni ngumu kwa hapa kutaja ugonjwa moja kwa moja ni upi ila nitataja baadhi ya hali/magonjwa ambayo yanahusisha dalili zinazofanana na hizo:
1. Rabies ( Kichaa cha mbwa)
2. Heartwater (maji kwenye moyo)
3. Listeriosis/circles (ugonjwa wa kuzunguka)
4. Encephalitis ( sina kiswahili chake)
5. Meningitis
6. Cerebral babesiosis
7. Cerebral ECF
8. Sumu aina ya Strychnine
.................
1. Rabies husababishwa na virusi(Lyssa virus) ni ugonjwa hatari wa kichaa cha mbwa huwapata sana mbwa lakini unaweza wapata pia paka,mbuzi,ng'ombe,kondoo na binadamu. Ugonjwa huu husambaa kwa ama kung'atwa na mbwa mwenye ugonjwa tajwa au mate ya mbwa aliyeathirika kugusa kwenye kidonda au sehemu za wazi za mwili za mnyama, kuzungukazunguka ni moja ya dalili ya Rabies.
2. Heartwater husababishwa na "Cowdria ruminantium" ni ugonjwa ambao husababisha maji kwenye moyo vijidudu hushambulia seli za mishipa ya damu nakupelekea kufuja kwa maji maji hatimae maji kujaa kwenye kuta za moyo, vijijidudu hivi hushambulia hadi mishipa ya kichwani (ubongo) na kupelekea dalili ya kuzungukazunguka.
3.Listeriosis ni ugonjwa unaosababishwa na bacteria aina nyingi ambao hushambulia seli za ubongo na kupelekea meningitis au encephalitis ambazo huleta dalili ya kuzungukazunguka.
4. Cerebral ECF, Cerebral babesiosis na sumu ya Strychnine huathiri mfumo wa ufahamu na kusababisha hali kama ya degedege na kuzungukazunguka.
Mimi pia siko mbali sana na wachangiaji wengine napendekeza magonjwa mawili kati ya yote hapo juu;
1. HeartWater (maji katika moyo) na
2. Listeriosis/ circles (kuzunguka)
Magonjwa haya hutibiwa kwa kutumia Antibiotics endapo yatagundulika mapema ila ukichukua muda ni ngumu kutibika.
Nakushauri utafute mtaalamu wa mifugo aliyekaribu na wewe akusaidie, matumizi ya ovyo ya Antibiotics, pasipo utaalamu huleta usugu wa magonjwa.