Msaada, Ugonjwa wa ngozi unaotesa Wanangu

zhang laoshi

JF-Expert Member
Joined
Aug 2, 2014
Posts
434
Reaction score
581
Habari Team
Poleni na majukumu, watoto wangu Wana Ugonjwa wa ngozi wanajikuna na kutokea vidonda na kuacha makovu meusi.

Nilifika hospital nikaambiwa na alegi waache kutumia ,mayai, nyama, maziwa na vitu vya sukari.

Niliacha kuwapa lakini bado watoto wanajikuna na kuacha makovu

Naombeni kujuzwa hata dawa za mitishamba ziwasaidie.

Asanteni
 
Huo ugonjwa hua unatoweka wenyewe maana upo kwenye damu Ila kikubwa zingatia ulivyoelezwa na madaktari kuhusu Vyakula nna mpwa wangu nae alikua na huo huo ugonjwa akawa anajikuna sana yanatoka hadi kichwani Sasa hivi umetoweka hana tena hio shida,

Kingine ni mafuta unayowapakaa wapakae mafuta ya Nazi sio mgando wala lotion wala cream wala mafuta gani sijui mnayopenda kujipaka msiwapakae watoto mnawasababishia matatizo ya Ngozi, Anza na mafuta ya Nazi yanaitwa Parachute dukani yanauzwa Bei rahisi sana

Mafuta ya Nazi yanatibu Ngozi na magonjwa ya Ngozi sijui wenyewe wanaita Pumu ya Ngozi sijui ndio hio ukipaka mafuta ya Nazi na ukaacha kumpa Vyakula ambavyo kila akila anaanza kujikuna unatoweka wenyewe huna haja hata ya kumpeleka kwenye maombi
 
Amabhundujo.
Mnaita tetekuwanga mkuu.
Nenda duka wanalouza madawa ya mifugo,waambie wakuuzie permanganate.
Kiasi kidogo tu,sijui ulipo lkn hometown ya 2000/- utatumia na ikabaki kwani kwenye nusu lita ya maji safi unaweka kiasi kisicho jaa kijiko cha chai.

Ukisha loweka itatokea rangi ya zambarau,sasa mtumiaji anapomaliza kuoga afanye km anatumia huo mchanganyiko kujisuuza mwili mzima.

Ni kwa ajili ya ngozi tu mkuu asinywe wala kuonja,afanye hivyo asubuhi na jioni ili kutoa muda wa dawa kutenda kazi.
 
Hao madokta wamezingua, allergy sio kitu specific kama hivyo et mayai n.k allergy inatofautiana mtu na mtu, angalia patterns ya kitu ambacho akitumia kinazidisha, it might take sometime.

Wakwangu tulienda tulitumia gharama sana kila dokta alisema lakwake, ni kweli ilikua ni allergy lakini yeye yakwake ilikua akila parachichi, ilichukua muda kufahamu, hadi sasa amepona ni makovu ndo yanaishia ila tatizo limeisha bila dawa yoyote
 
Naona kila mmoja anasema lake, na humu sisi sio madaktari. Tunapotoshana tu hapa.
Mhusika aende tu hospitali kubwa kubwa na kuonwa na madaktari wa ngozi huenda akapata suluhisho kamili.
 
Kama usiku ndiyo wanawashwa sana itakuwa scabies....nenda kwa speacilist wa ngozi...kama ni scabies itabidi nyumba nzima mpake dose...na kufanya bonge la usafi...madogo wangu waliambukizwa na aunt yao alipotoka boarding school...madogo waliteseka sana maana na wenyewe waliambiwa mambo ya pumu ya ngozi....scabies ni kama kunguni wa ndani ya ngozi ...noma sana aisee
 
Nunua BBE
Kichupa inapakwa joini akilala jumamosi na jumapili, usimpake tena baada ya hiyo awamu then rudia weekend inayofata wapake tena wote. Hata ninyi kwa sabab unaambukiza.

Umenitesa sana familia.

Mtoto mchanga dilute usimpake kama ilivyo.

Fungus nguo isirudiwe na ikaule au ipigwe pa's la maana.

Mm umepotea kwa njia hiyo.


Kuhusu vidonda, usipake sehem zenye vidinda. Nunua silverrex tube paka kwenye vidonda tu.
 
Hao watoto wapo hivyo kuna Vyakula akila anaanza kujikuna Mwili mzima tena ukikuta Cha kike kinajikuna huku kinalia Sasa mzazi inabidi umjue mwanao chakula gani nikimlisha anapatwa na hali hii mfano Samaki au nyama wengine wakila tu wanaanza kujikuna au Vyakula vya ngano ngano km Tambi akila tu anaanza kupiga gitaa Mwili mzima
 
Hata ninyi kwa sabab unaambukiza.
Huo ugonjwa hauambukizi hata kidogo mkuu yaan mtoto alionao ndio utamsumbua yeye tu watoto wengine au hata wewe unaweza umshike na umuhudumie na usikupate hata Mama yao hauwezi kumpata pamoja na kwamba anawahudumia, watoto anaweza hata kucheza nao na asiwaambukize Ila yeye tu ndio unamsumbua, sio wa kuambukiza
 
Huo ugonjwa hauambukizi hata kidogo mkuu yaan mtoto alionao ndio utamsumbua yeye tu watoto wengine anaweza hata kucheza nao na asiwaambukize Ila yeye tu ndio unamsumbua, sio wa kuambukiza
Kama ni scabies wanaambukiza haraka sana
 
Madokta ndio hawa wanaovaa milegezo na kuchati whatsapp ofisini?

Hao watoto kuna kitu unawalisha wewe sio bure!! Kama sio SODA au yale MAJUICE ya ajabu ajabu ya kwenye vikopo.

Au kuna mavyakula yenye sumu unawalisha mpaka kinga ya mwili inatetereka.

Na ukichunguza zaidi kuna MADAWA unawalisha, au UMEWADUNGA MACHANJO yale yaliyojaa sumu tupu.

Utadanganywa sana na hawa madaktari uchwara waliosoma kwa kukariri vitini, utalishwa madawa mpaka uombe poo.

Hayo mapele yanaashiria kuna kitu hakiko sawa ndani ya mwili. SUMU NA UCHAFU umejaa ndani ya mifumo.

Na hauwalishi chakula stahiki. MAJANI NA MATUNDA huwapi. Unawalisha maugali na manyama tu.
 
Umetumia BBE?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…