Msaada, Ugonjwa wa ngozi unaotesa Wanangu

Msaada, Ugonjwa wa ngozi unaotesa Wanangu

Madokta ndio hawa wanaovaa milegezo na kuchati whatsapp ofisini?

Hao watoto kuna kitu unawalisha wewe sio bure!! Kama sio SODA au yale MAJUICE ya ajabu ajabu ya kwenye vikopo.

Au kuna mavyakula yenye sumu unawalisha mpaka kinga ya mwili inatetereka.

Na ukichunguza zaidi kuna MADAWA unawalisha, au UMEWADUNGA MACHANJO yale yaliyojaa sumu tupu.

Utadanganywa sana na hawa madaktari uchwara waliosoma kwa kukariri vitini, utalishwa madawa mpaka uombe poo.

Hayo mapele yanaashiria kuna kitu hakiko sawa ndani ya mwili. SUMU NA UCHAFU umejaa ndani ya mifumo.

Na hauwalishi chakula stahiki. MAJANI NA MATUNDA huwapi. Unawalisha maugali na manyama tu.
Hapa ndio umesaidia nini?
 
Mwanangu aliwahi kupata tatizo kama hili nilizunguka hospitali zote hapa dar, kuna dr mmoja anaitwa massawe pale morocco akasema akifikisha miaka mitano itaisha na ni kweli sasa ni kijana mkubwa hana shida tena.
 
Habari Team
Poleni na majukumu, watoto wangu Wana Ugonjwa wa ngozi wanajikuna na kutokea vidonda na kuacha makovu meusi.

Nilifika hospital nikaambiwa na alegi waache kutumia ,mayai, nyama, maziwa na vitu vya sukari.

Niliacha kuwapa lakini bado watoto wanajikuna na kuacha makovu

Naombeni kujuzwa hata dawa za mitishamba ziwasaidie.

Asanteni
Chukuwa hii lakini badae usifanye kama unauza kwa watu yaani waambie bure kabisa kama mimi ninavyokwambie.

Tafuta mti wa mwarobaini mizizi yake

Tafuta mti wa mjohoro mizizi yake

Tafuta mbaazi mizizi yake huu unachimba mzizi asubuhi saa kumi na moja hakikisha usemezani na mtu au haupo katika siku zako kama ni kwanamke, vile vile hupaswi kuwa na jasho la kufanya mapenzi.

Tafuta mzugwa majani yake.


Chemsha kisha muogeshe mtoto/watoto asubuhi na jioni changanya na chumvi ya mawe.

usichanganye na maji mengine kabisa.

mwarobaini
Mjohoro
Mbaazi
Mzugwa

mpatie kikombe nusu kimoja kila siku usichanganye na chumvi ya mawe katika kuvywa.

Matumizi ni siku saba za mwanzo kisha unaacha siku saba nyingine haumpi.

Siku saba nyingine unampa siku saba nyingine unaacha

Siku saba nyingine unampa,hapo atakuwa kamaliza dozi.

Mana hiyo hutumika kwa mara tatu katika mfumo huo.

HIVYO NDIO NIJUAVYO TIBA HIYO.

Onyo😡 mimi sio mganga usinifate pm tafadhali 😂
 
Habari ..
Angalia vitu hivi ni lini mara ya mwisho umewapa dawa ya minyoo?,chunguza hiyo shida inatokea hasa baada ya kula au kunywa nini? Kwa maana kwamba wanaweza kuwa na allergy na baadhi ya vyakula pia kapime ujue kama wanamchafuko wa damu..
 
Pole sana, huo unaitwa ukurutu, scabies kitaalamu.. Ni bora uende hosp nyengine wawaangalie vizuri ili wote waanze matibabu ikiwezekana na wewe mwenyewe kama umekupata pia.
Umetumia kigezo Gani kusema ni ukurutu.
 
#Mrejesho#

Habari za Mida wakuu, napenda kutoa mrejesho wa Ugonjwa huu unaosumbua watoto wangu.

Nashukuru Kwa wote mliotoa ushauri juu ya hili tatizo asanteni sn

Shida ni Maziwa fresh ya ng'ombe , nilikuwa nawanunulia mtindi maeneo ya Mbezi, sasa nikaja kununua Maziwa fresh ya ng'ombe katika kabisa moja hapa mtaani. Hapo ndipo tatizo lilipoanza Kwa Kasi Ila baada ya kuacha kuwapa naona vinaanza kupungua na wanaacha kujikuna.

Nimepanga kuendelea kufatilia vitu vingine vinavyoweza kuwapa allergy pia nimembiwa hata mayai ya kuku yanaweza changia.

Ila Dr kaniambia wakifikisha miaka 5 kuna possibly ya ugonjwa huu kuisha

Asanteni
 
Habari Team
Poleni na majukumu, watoto wangu Wana Ugonjwa wa ngozi wanajikuna na kutokea vidonda na kuacha makovu meusi.

Nilifika hospital nikaambiwa na alegi waache kutumia ,mayai, nyama, maziwa na vitu vya sukari.

Niliacha kuwapa lakini bado watoto wanajikuna na kuacha makovu

Naombeni kujuzwa hata dawa za mitishamba ziwasaidie.

Asanteni
Nitafute WASSAP 0779427472 Kila kitu kinaenda kuisha kabisa
 
Back
Top Bottom