Msaada ulevi unanitesa

Msaada ulevi unanitesa

rubii

JF-Expert Member
Joined
Feb 22, 2015
Posts
14,032
Reaction score
18,540
Habari zenu wakuu

Nimekua na mambo yananisumbua zaidi ya mwaka sasa, na nimeweza kuwa mnafki na kuyaweka moyoni tu bila kuongea kwa watu mambo hayo.

Kutokana na mambo mengimengi nilijikuta siwezi kulala usiku bila kumeza dawa(piriton)

Mwanzoni nilichukulia kawaida lakini sasa naona hali inazidi kuwa mbaya zaidi nilianza na vidonge viwili sasa nimefikia vitano.

Kila siku usiku ni lazima nimeze vidonge hivyo kama nahitaji kulala na vimekua msaada mkubwa kwangu

Lakini sasa vinanitesa, Mapigo ya moyo yanaenda mbio mda wote natoka jasho kama glass iliyotolewa kwenye jokofu, Nahisi kizunguzungu mara kwa mara na giza la gafla hata imefikia kuanguka anguka.

Ndugu wamekua wakiulizana nini tatizo nashindwa kuwaelezea tabia yangu ya kubwia mavidonge kila usiku, na nisingependa watu wafahamu napitia nini katika nafsi yangu.

Nifanyeje niweze kuacha matumizi ya dawa hizi??

Je nikiendelea na ulevi huu nini mwisho wangu??

Pole sana ndio maana ulibadilika ghafla, nilikupenda sana b4 lakini nilivoona mapichapicha moyo wangu nikauondoa fasta.

Kwa ushauri zaidi muone Dr. Daud atakusaidia maana amesaidia wengi.

Dr Daudi anapatikana wapi mpendwa??

Ungeandika hapa hilo tatizo upewe msaada wa mawazo huo ndo ungekuwa mwanzo wa tiba yako hafu punguza kumeza piritoni aisee mi nikimeza moja huwa nakuwa hoi kabiss

My dear, hii shida ni ya kiroho zaidi.
tatizo bila piritoni siwezi kulala kabisa akili yangu inakuwa busy kuwaza

My dear, hii shida ni ya kiroho zaidi.
tatizo bila piritoni siwezi kulala kabisa akili yangu inakuwa busy kuwaza
Ka ni mkristo funga uwe una sali kuhusu hilo tatizo litaisha kabisa, kuna kipindi nilipitia kipindi kigumu sana kwenye life I lost hope and nilikuwa ka nachaganyikiwa nikaamua kufunga na kusali tatizo likaisha, kufunga hata kusali hutupa nguvu sana kuna mambo kwa akili zetu Ku handle ni shida sana.

Habari zenu wakuu

Nimekua na mambo yananisumbua zaidi ya mwaka sasa, na nimeweza kuwa mnafki na kuyaweka moyoni tu bila kuongea kwa watu mambo hayo.

Kutokana na mambo mengimengi nilijikuta siwezi kulala usiku bila kumeza dawa(piriton)

Mwanzoni nilichukulia kawaida lakini sasa naona hali inazidi kuwa mbaya zaidi nilianza na vidonge viwili sasa nimefikia vitano.

Kila siku usiku ni lazima nimeze vidonge hivyo kama nahitaji kulala na vimekua msaada mkubwa kwangu

Lakini sasa vinanitesa, Mapigo ya moyo yanaenda mbio mda wote natoka jasho kama glass iliyotolewa kwenye jokofu, Nahisi kizunguzungu mara kwa mara na giza la gafla hata imefikia kuanguka anguka.

Ndugu wamekua wakiulizana nini tatizo nashindwa kuwaelezea tabia yangu ya kubwia mavidonge kila usiku, na nisingependa watu wafahamu napitia nini katika nafsi yangu.

Nifanyeje niweze kuacha matumizi ya dawa hizi??

Je nikiendelea na ulevi huu nini mwisho wangu??
Polee mpendwa Rubii nadhani kama utaweza kumpata mtu ukaweza kushare nae hilo jambo itakuwa tiba mojawapo,
Halafu kama unaweza fanya mazoezi na uchoshe mwili uone kama pia bado utakuwa hupati usingizi.

pole mamy natumaini utapata washauri wazuri.. lakini dawa kubwanikujifunza kupuuza na kuacha mambo yapite kama unakosa usingizi sababu ya jambo ila kama imetokea tu basi pole na nenda hospital.. kukosa usingizi ni dalili mojawapo kati ya jingi ya kuwa chizi ila i hope utapona

Pole sana ,inaonekana una msongo wa mawazo ndio maana lazima unywe dawa ndio upate usingizi.Ushauri ni kutafuta solution ya matatizo yanayokukabili ili ubongo upumzike wakati wa usiku mkuu.

Jamani...
Hivi JF siku hizi imekuaje..!?
Wataalamu wameenda wapi..!?
Hadi sasa hivi sijaona mtaalamu yeyote aliyetoa maelezo kwa dada rubii kuhusu side effects za matumizi ya piriton yaliyopitiliza..!

Pole sana! Kama kuna rehab za mambo hayo hapa Tanzania inabidi ujipeleke. Unahitaji msaada na si rahisi kuacha peke yako

mimi nadhani usikae na jambo moyoni litakutesa maana hata mimi nakumbuka mwaka jana nilipata tatizo ambalo nilikuwa silali mpaka ninywe sana, nimekaa nalo moyoni huku naumia sana, nilienda kwa wataalamu wakaniambia mbona umekaa nalo moyoni limekutesa hivyo mpaka umeisha, walinishauri vizuri sana mpaka hivi sasa pombe nakunywa kama starehe na wala si kwa sababu ya stress, matatizo yameisha, usingizi napata vizuri na afya imetengemaa, usikae na neno huo ndo ushauri wangu

Pole sana ndugu.
Ila mimi huwa nikimeza piriton sipati usingizi ni kama sijameza kitu kabisa.

Jamani...
Hivi JF siku hizi imekuaje..!?
Wataalamu wameenda wapi..!?
Hadi sasa hivi sijaona mtaalamu yeyote aliyetoa maelezo kwa dada rubii kuhusu side effects za matumizi ya piriton yaliyopitiliza..!

nadhani wataalamu wetu wapo busy na MMU kama sio bashite maana sio kwa ukimya huu

Fanya haraka nenda kwa counselors. Yaani kifo unacho soon very soon. Tafuta hata mti uongee nao shida yako

Back
Top Bottom