mimi nadhani usikae na jambo moyoni litakutesa maana hata mimi nakumbuka mwaka jana nilipata tatizo ambalo nilikuwa silali mpaka ninywe sana, nimekaa nalo moyoni huku naumia sana, nilienda kwa wataalamu wakaniambia mbona umekaa nalo moyoni limekutesa hivyo mpaka umeisha, walinishauri vizuri sana mpaka hivi sasa pombe nakunywa kama starehe na wala si kwa sababu ya stress, matatizo yameisha, usingizi napata vizuri na afya imetengemaa, usikae na neno huo ndo ushauri wangu