Binafsi nimesoma bandiko la mtoa maada kisha nikasoma comments zote za wadau, halafu nikarudia kusoma tena andiko in a very sympathetic manner, KUSEMA UKWELI, nadhani ambao wametukana au kukejeli na kumdharirisha mtoa maada hawapo fair hata kidogo. Ni bahati mbaya sana daima tunatanguliza empathy yaani kuangalia tatizo la mtu mwingine tukiwa mbali bila kujaribu kuvaa tatizo hilo sisi.
Kuna mtu aliwahi kuandika kwamba, ukiona mtu ameamua kumweka mtoto mtoni/majini basi ujue mtu huyo ameona mtoni ni sehemu salama kuliko nchi kavu. KUTOKA 2:3 Musa aliwekwa mtoni na mama yake akijua ataokotwa na kulelewa.
Mtoa maada ameandika kwa hisia zinazoonyesha anaupendo kwa mwanae na ndiyo maana amesema mda mwingi anashinda naye ila wakati mwingine anatoka kwenda kutafuta riziki hivyo KULAZIMIKA kumwacha mtoto.
Ameomba kama kuna mtu anaweza kumsaidia kumlea mtoto “anaamini” mtoto ni wa jamii nzima ila kama hatapatikana msamaria mwema basi walau awepo wa kumchukua na kumlea kama mwanae ili TU MTOTO AISHI. Huu ni upendo mkubwa kwa mtazamo wangu.
Binafsi nimewahi kupitia changamoto kipindi fulani nikiwa hapo Dar, Mungu pekee ndo anajua, nilijifunza sana na hadi sasa siwezi kumwona mtu mwenye changamoto za kiuchumi kama mzembe na kuanza kumtusi bila kumfahamu in and out.
Huu ni mtazamo wangu tu. HOWEVER, Suala la kumtoa mtoto si kubaliani nalo sana unless that’s the only option left. Nimewahi kufundisha shule sasa kulikuwa na binti wa kidato cha tatu aliyekuja kugundua kuwa alikuwa adopted na wazazi wake hawafahamu, aise japokuwa alikuwa smart form one na two kabla hajafahamu siri hiyo, hali hili ilimwathiri kiasi kwamba kila mmoja pale shule alishangaa jinsi alivyobadilika kutoka mwanafunzi bora hadi kuwa duni wa kwanza darasani.
NDUGU YANGU MUNGU NI MWEMA SIKU ZOTE, NAAMINI KUNA SIKU ATAKUFUNGULIA NJIA NA UTAWEZA KUTOKANA NA CHANGAMOTO HIZO, MWISHO KAMA HUTOJALI NAOMBA UNI PM TUONE NAMNA YA KUSAIDIANA KWA NAMNA YOYOTE.
Aquila non capit muscas!