Msaada unahitajika wa haraka Tafadhali!! Katika hii Biashara ya KUKU

mjasilia

JF-Expert Member
Joined
Aug 25, 2012
Posts
594
Reaction score
172
mimi nimgeni katika hii biashara ya kufuga kuku; nimeanza kama nina wiki moja ivi; hawa kuku nimewanunua kutoka maeneo mablimbali ila wamefika nyumbani kwa siku mbili tofauti wakitoka sehemu tofauti siku ya nne nikashauriwa na watu kuwa niwape chanjo ya newcastle, nikawanunulia na kuwapa ile ya kidonge, siku moja tu baada ya kuwapa chanjo wapatwa na ugonjwa ambao una kila dalili ya kuwa ni mdondo, nimejaribu kila njia kwa kuwapa alovera, tetlecekilini, sasa hivi ndiyo nawapa dawa ya antibiotic nimeenda ubungo nikamwaona dk wa mifugo akasema nilikosea kuwapa chanjo ya mdondo kabla ya kuwapa antibiotic kasema hii chanjo kama kuku ana ugonjwa tayari huwa inautibua na kusambaa kwa kasi aksema wanaweza kufa wote nimeogopa ndugu yenu tena sana.

hawa kuku ni wakubwa matetea kama ishirini na majogoo watatu, wamenigharimu kama lako 350000 mpaka sasa , jamani mimi nimetafuta kazi sijapata mwaka wa pili nikaamua nijifungulie kimradi cha kuku hii pesa nimeitafuta kwa muda miezi kama 8, hivi kusudi likiwa nijiajilianagalau mimi ni graduate wa tourism and cultural heritage! nisaidieni ushauri na msaada wa ku rescure hawa kuku ambao ni tumaini langu
 
Aisee pole sana, mimi sina uzoefu wa ufugaji, jamani mwenye uzoefu msaidie mkuu
 

usingewapa dawa bila ushauri wa daktari,so cha kufanya hapo inabidi utafute mahali ambapo huwa wanavipasua mfano pale ubungo kuna daktari anaitwa dr madunga ni mzur sana peleka kimoja atakipasua,atakipima then atakupa jibu la tatizo,halafu kama ni wa kisasa jitahd sana kuwa close nao kwenye uangalizi,vinginevyo watakutia hasara
 
wakorogee maji ya sukari ...weka sukari kilo moja kwenye lita tano.
pole sana aisee...
 
ni wakubwa siyo vifaranga pale ubungiodkta kasema kuku kama alikuwa anaumwa nimekosea kumpa chanjo kabla ya antibiotic, kaniambia ni dalili za mdondo wanaharisha maji na mchanganyiko wa njano , ila kuku wa kienyeji!
asante kwa ushauri natka hasa jinsi ya kuzuia kuwaepusha na hasa tatizo la kuharaisha maana wanaishiwa nguvu sana!
 
nimenunua glookoz ya kuku na wakati huo huo nawapa dawa fulaniivi antiobitic nimepewa na dokta wa mifungo pale ubungo! unakuta jogoo mkubwa aina ya kuchi ameregea mpaka ninalia aisei ! asnte kwa ushauri nitafanya hivyo kesho asubuhi maana kwsasa awataweza kunywa labda niwanyeshwe!
wakorogee maji ya sukari ...weka sukari kilo moja kwenye lita tano.
pole sana aisee...
 
Pole kwa wakati mgumu unaopitia, KUMBUKA, ukishindwa kuwaokoa wakafa wote haiwezi kuwa mwisho wa maisha yako. Mungu anaweza kukupa fursa nyingine. Wajasiria mali wote wanapitia hatua kama hiyo unayopitia wewe. Hata hivyo, fuata ushauri unaopewa inawezekana ukawaokoa kuku wote au baadhi yao. Usiogope mkuu.
 
Search humu ndani au google topics za ufugaji wa kuku zipo nyingi humu.
 
asante kaka, nachelewa kuwa jibu macho yote yameelekezwa bandani..!
 
asanteni kwa msaada wa ushauri mnaonipatia nitajaribu kwa kila namna mbarikiwe!
yap yap...mimi kipindi nimemaliza chuo nimefuga kuku sana..tena nilikuwa na hela kuliko sasa..basi tu maisha
 
unatakiwa uwalishe na kuwanywesha mmmoja mmmoja kila saa na kijiko
 
kosa kubwa sana kuanza ufugaji bila kujipanga na wataalam......pole.....anyway..vyovyote itakavyokuwa chukulia ni mojawapo ya changamoto nyingi utazakazokutana nazo..usikate tamaa!!tumepitia humohumo!!!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…