MSAADA; Upimaji wa Maji na Udongo kwa ajili ya kilimo biashara

MSAADA; Upimaji wa Maji na Udongo kwa ajili ya kilimo biashara

The Saver

JF-Expert Member
Joined
Aug 21, 2014
Posts
202
Reaction score
651
Ndugu zangu wanaJF

Nina shamba langu nimejiandaa kwa kilimo biashara nimeishakusanya vifaa vyote vya kilimo

Shamba langu lina ukubwa wa ekari 4 nimeishapata drip irrigation za kutosha na vitu vingine maana nimeapply kazi mpaka sasa mwaka hakuna cha ajira

Sasa nimekwama sehemu ya upimaji udongo na maji kwa hapa DAR ES SALAAM, nimejaribu kuulizia wengi wanapeleka SUA, Wengine KENYA, Wengine wanawapa watu binafsi wanawapelekea kupima (hapa kwa watu binafsi unaweza kuhujumiwa maana unaweza kuletewa report tofauti)

Je hapa DAR ES SALAAM NAEWEZA PATA KAMPUNI AMBAYO NAWEZA KUPELEKA UDONGO NA MAJI YANGU MWENYEWE BILA KUPITIA KWA DALALI?

Msaada
 
Kwa dar cjajua Arusha Selian,Tanga mlingano na sua morogoro ndio pekee kwa tanzania ndg ila kama kuna vpya utajuzwa na wadau
 
Hongera sana kwa jitihada zako....nenda pale wizara ya maji ubungo pale....wala hauitaji dalali...ada zao ziko pale....wana maabara....utafanyiwa unachotaka bila longolongo....
 
Hongera sana kwa jitihada zako....nenda pale wizara ya maji ubungo pale....wala hauitaji dalali...ada zao ziko pale....wana maabara....utafanyiwa unachotaka bila longolongo....

Wizara ya maji ipo sehemu gani kwa ubungo au unaimanisha pale chuo cha maji njia ya kuelekea udsm?

Nashukuru sana
 
Kwa dar cjajua Arusha Selian,Tanga mlingano na sua morogoro ndio pekee kwa tanzania ndg ila kama kuna vpya utajuzwa na wadau

Nashukuru sana kwa ushauri lakini arusha, tanga na morogoro kuna umbali lakini ikobidi itabidi niende
 
Nenda chuo cha maji ubungo wanapima maji na kutoa hati, wanazo maabara na wataalamu wa kutosha.
 
Inatizamana na makao makuu ya tanesco...

nashukuru sana nitaenda hapo J3

Kama una uzoefu nielekeze nende idara gani maana kama ni wizara itakuwa na ofisi nyingi

Nashukuru saana kwa msaada wako
 
Ni rahisi sana pale....hapana complications...ukiingia tu unawakuta walinzi....waulize maabara ilipo...off u goo....!!
 
Hivi pamoja na kelele zoote zile "kilimo kwanza" hata maabara za kupima udongo na maji ni shida!? Kweli wanasiasa ni wasanii nambari wani!
 
Nashukuru sana kwa ushauri lakini arusha, tanga na morogoro kuna umbali lakini ikobidi itabidi niende

Ucjal ndg muhimu ujue ph ya maji nj wadudu na magonjwa,usisita kupima udongo pia kwa ushaur coz I'm horticultrist by proffesional
 
Back
Top Bottom