Msaada ushauri kuhusu nissan murano

ukinunua Murano utajutaa, yaani utajuta utapata magonjwa yote ya moyo, presha, stress na kuongea mwenyewe barabarani.
kwa ufupi;
- kwenye murano kuna tatizo la transmission failure na hadi uje kutibu huu ugonjwa utapungua kilo 5.
- kuna tatizo la transfer case kufail na hadi uje kutibu huu ugonjwa utapungua kilo 10
- kuna tatizo la mfumo wa umeme kufail Mara kwa Mara, na hadi uje kutibu huu ugonjwa utapungua kilo 15.
hvyo kwa ujumla ukiwa na murano kuna probability ya kupungua kilo 30 kwa matatizo utayokumbana nayo
Murano vitu Vingi vilikosea hvyo kuleta shida kwa watumiaji hasa wa huku ulimwengu wa tatu(3rd world).
Usichukue hiyo murano, tafuta nyingine
 
Naomba ushauri mimi ke sio me
Ngoja aje wifi ako akushauri, mi hata sielewi aliipendea nin hiyo gari though sikuhizi hazionekani kabisa barabarani zimepotea kama vile Xtrail and I'm 100% sure there must be something not ok with it.
 
mkuu njoo tuongee Murano mbichi kabisa namba DFC ipo dar 0719308160 na haina tatizo lolote
 
Nataka chukua hii gari naombeni mnipe ushauri wadau
Nissan Murano kama magari mengine, ni ya kawaida ila matunzo ndio muhimu. Usibabaishwe na wasioelewa, gari hii imeuzwa kwa wingi sana na bado zipo barabarani.
Cha msingi ni kuzingatia service na kutumia genuine parts and lubricants. Fundi wako poa lazima awe anaelewa kazi yake na sio kujaribu jaribu. La kwanza lazima ujue wapi utaifanyia diagnosis ili kufahamu matatizo KABLA ya kwanzia ukarabati; hata hospitalini lazima ukapimwa kabla ya kupasuliwa, hawakupasui ili kuangalia prblm!
 
Mkuu, kitu kuzuri ghari pia kukitunza. Nissan Murano ni gari nzuri, class ya BMW na Macedez Benz. Inatulia barabani, fuel consumption nzuri, ila haitaki shida, na spear ghari kidogo, kama umezoea gari poa poa hii itakusumbua.
 
Hujasema hiyo Nissan Murano unayoikandia sana kwenye post yako ni toleo/model (mwaka) gani? Magari huwa yana improve baada ya kila toleo. Nissan Murano ya 2006 siyo sawa na Nissan Murano ya 2010. Be objective, usifikiri kila mtu ni mbumbumbu. La ziada: experience ya mtu mmoja na gari lake haimaanishi kila gari itakuwa na matatizo hayohayo. Watu wanatofautiana sana kwa matunzo (maintenance) na uendeshaji wao.
 
Kabla hujaagiza angalia taa ya check engine, nyingi taa zimewaka kuashiria tatizo, ila kama utatumia mwenyewe zingatia service na oil sahihi,
 
Nimeshauriwa kununua matairi makubwa au Kunyenyua gari, kipi bora? Gari yangu n Honda Fit.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…