Kamanda Kazi
JF-Expert Member
- Dec 15, 2012
- 2,613
- 795
Hebu ndugu zangu naombeni ushauri na maoni yenu katika hili. Katika nchi zingine mtunzi anaweza akatunga script ya mchezo wa sinema/maigizo au nyimbo, akatunga kitabu, nk na kisha kazi hiyo akaiuza kwa mtu mwingine na kutengeneza kipato. Sasa sijui kwa Tanzania kama hili linafanyika pia na je, lina tija kwa mtunzi? Au mtunzi akatunga kitabu lakini akawa hana fedha ya kukichapa na kukiingiza sokoni lakini akaingia mkataba na kampuni au mtu mwingine ambaye atafanya kazi hiyo ila wakagawana mapato kwa mujibu wa makubaliano.
Binafsi nina vitabu vitatu (03) nimetunga lakini kwa sasa sina mtaji wa kuvichapa na kuviingiza sokoni ila natamani ama ningepata mtu wa kununua kazi yangu au ambaye nitaingia naye mkataba tukalipana kazi ikitoka.
Hivyo nahitaji maoni na ushauri wenu hapa jamvini na atakayependa anipigie
katika simu +255 688 308840 au kwa Email: alex.peter_75@yahoo.com