Msaada: Ushauri machine ya uzalishaji

Nyamburi

JF-Expert Member
Joined
Oct 28, 2011
Posts
306
Reaction score
36
Wadau habari!nakuja jamvini hapa kuomba ushauri wenu. Nina wazo la kununua machine ndogo kwa ajili ya production,budget yangu ni kati ya 5m/= mpaka 8m/= kwa ajili ya ununuzi wa machine hiyo,ila katika wazo langu nimekosa kujua ni machine ya kitu gani hasa ambayo nikinunua bidhaa zake hazitakua kikwazo sana katika kuuzika!naomba kwa wadau wenye uwezo wa kunisaidia mawazo wanisaidia tafadhali,Asanteni wadau
 
Duh we kwel unahtaj msaada

Sasa mkuu hapo unaona umemsaidia au?jamaha mbona ameomba ushauri wenye tija tu,tusivanjane moyo bali tupeane courage kwa yale ya msing!mkuu Nyamburi,me nakushauri jaribu kutafuta machine za kutengeneza vitu kama chaki au hata mifuko ya ice cream/nylon,sijajua bei zake zikoje ila nina hakika ni affordable na bidhaa utakazo zalisha zinatumika daily
 


Mkuu inaonekana una ela lakini hujui uitumie je, kwanza kabisa wewe unadhani ni mashine ipi ungependa uwe unaimonitor???
 

Hizo ni baishara za mtaji wa 50000 bora anunie mashine za kusaga aende mbeya huko
 
Ndugu uja ainisha ni msaada wa machine ya aina gani unataka yakusaga ya kukoboa ama ya kupukuchua mahindi
 
Hizo ni baishara za mtaji wa 50000 bora anunie mashine za kusaga aende mbeya huko

Mkuu kumbe idea nzuri ulikua nayo,hata mimi niliwaza ilo,japo haja ainisha hiyo kitu anataka afanyie wapi,ila kama ni mikoani hasa ile mikoa inayolima nafaka,ukweli akiweka machine ya kukoboa na kusaga,atapga hela nyingi tu
 
Nami naungana na wadau waliotoa wazo la machine ya kusaga na kukoboa!hii kitu nimeshuhudia mwenyewe ikiwatoa watu kwenye ufukara mpaka kwenye uhakika wa maisha,ila hii biashara haifai kwa mji kama wa Dar,ukiwa wewe ni muajiriwa basi tafuta mtu muaminifu muweke mikoan hasa Mbeya,Rukwa au Morogoro na uwe unakoboresha na kusaga,ikiwezekana weka na viroba vya kilo 5 na 25 uwe unasagisha mwenyewe na kuuza kwa jumla na reja reja!ndugu hii itakusukuma sana,cha msingi ni ufuatiliaji,kama huko Dar na ni muajiriwa bora uweke machine Moro maana hapa ni karibu sana kwa ufuatiliaji,na ni rahisi kwa wanunuzi wa jumla toka Dodoma na Kibaha kukufikia!hzo machine za mifuko na chalk me siungi mkono sana maana zitakusumbua
 

Nenda hapa www.zhauns.com kuna kila aina ya mashine kwa ajili ya mjasiriamali. Hutakosa wazo na itakayo kufaa.

Mi niliagiza kwao mashine ya kutengeneza trays za mayai za mabox shemeji yenu mtarajiwa hajapata kazi tangu amalize chuo 2011 ila inamkeep busy mbaya hataki tena kuajiriwa.
 
Wadau asanteni sana kwa ushauri wenu,ukweli nimepata mwanga kidogo wapi naweza kuanzia,nimependa ushauri wa machine za kusaga mikoani na huyu mdau alienipa wazo la kutembelea tovuti ya Zhauns - Business Opportunity Machinery nawashukuruni sana wandugu
 

Asante sana kwa wazo lako na kunipatia link hii ndugu yangu,nimeitembelea kweli nimeona wana mambo mengi sana,ila naomba nikuulize kitu mkuu,je hizo tray za mayai shemeji yetu zinamlipa vizuri?nimeipenda hii,lakini sina uhakika na mkoa ninaoishi kama itakua ni biashara nzuri!asante
 

Je hizo mashine ni bei gani mkuu.
mfano ambayo unaweza kuzalisha mifuko ya plastiki.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…