Msaada: Ushauri wa kiufundi kabla ya kuagiza gari hizi

lucley

JF-Expert Member
Joined
Jun 15, 2016
Posts
727
Reaction score
1,986
Salaam wanajukwaa,

Baada ya kujaza kibubu kwa muda mrefu, hatimae nimeamua liwalo na liwe mwaka huu lazima nimiliki usafiri binafsi. Bajeti yangu mpaka sasa ni 15m. Baada ya upembuzi wa muda mrefu nimeangukia kwenye gari mbili zifuatazo, Nissan Dualis na Toyota Premio.

Matumizi yangu makubwa ni kazini, nyumbani na mizunguko ya mjini. Mazingira ninayoishi ni lami, ila kuna kipande cha takribani 1km cha rough road za mitaani (mwendo wa dkk 4). Pia natarajia kufanyia safari za Dar to Southern Highlands every once in a while.

NB: Ni gari yangu ya kwanza kumiliki, sina uzoefu wowote wa magari ila nina uzoefu wa mashine mbalimbali na technical know-how zake.

Natanguliza shukrani.
 
Kama ndio gari yako ya kwanza nashauri nunua Toyota Premio kwanza then ukishapata uzoefu wa magari baadae ndio utanunua Nissan Dualis. Ni hii kwasababu kuwa spare za Toyota Premio zipo nyingi sana na zinapatikana kwa bei nafuu kuliko Nissan Dualis japo tofauti yake ya gharama ya spare za magari hayo no ndogo ukilinganisha na kipindi cha nyuma.
Binafsi gari yangu ya kwanza nlinunua Premio mwaka 2015 nikaja kuuza mwaka 2020 ikiwa katika hali nzuri tu na mbadala wake nikanunua Nissan Dualis na Toyota Belta ambazo ninazo Hadi sasa. Na hiyo yote ni baada ya kupata uzoefu kupitia Toyota Premio ndio nikaja kununua gari hizo mbili.
Japo uamuzi wa mwisho unabakia kwako. Ila kama utakuwa na safari za mara kwa mara za kusafiri kwenda mikoani nashauri nunua Nissan Dualis kwakuwa ni gari ya juu hivyo itakufanya uwe comfortable unaposafiri kuliko Toyota Premio.
 
Shukrani mkuu, vipi kuhusu dualis haina magonjwa ya mara kwa mara, maneno kuhusu usumbufu wa gari za nissan mtaani ni mengi.
 
Both ni gari nzuri ila issue inakuja hapa, kwakua ni gari ya kwanza, unataka gari reliable, dependable, and durable, with low operational costs, nunua premio, baadae ukataka fancy nunua Dualis

Dualis au nissan kiujumla zinazokuja ni gear box ya super CVT zinazotengenezwa na jatco (supplier wa transmission system wa Nissan kawa outsourced) commonly zinakua na shida kuachia ngazi mapema kwa sababu cooling issues kwenye gearbox lakini pia inherent quality issues kwenye design ya CVT transmission zao.. so zinahitaji umakini kwenyw utanzaji na utumiaji.. but these issues huzikuti kwenye premio either yenye cc 1496 or 1700+ cc.. kwakua zote zinakuja na standard automatic gear box inayotomia ATF-type 4 fluid.

Pia Nissan Dualis na nissan nyingi za kileo zinakuja na mfumo wa umeme wa IPDM(intelligent power distribution module) this is self diagnostic Power distribution module but inaharibika haraka sana na ikiharibika mafundi wengi ww kibongo huwa hawezi kuponya... So unalazimika kununua fuse box nzima ya gari yako... Fuatilia watu wenye nissan Dualis wengi wanakutana na changamoto ya umeme hass kwenye mfumo wa Ac. So as beginner you don't want to be exposed to all these shits za nissan...
 
Ukianza na Premio utakapoamua kuiza inauzika haraka zaidi.
Ukishauza utaongeza pesa ununue hiyo Nissan.
Nissan ni gari zuri lakini hayajazoeleka na kukunalika kwa wengi, hivyo haiuziki kwa urahisi.
Kwa sasa nunua Premio.
 
Hapo jibu ni moja tu aelekee Aichi Japan. Hapo panapounda Toyota Premio ni gari very comfortable kwa mtu anayeanza kumiliki gari kuanzia costs zake za uendeshaji mpaka maintanance
Heshima yako kiongozi, nimekuelewa.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…