Msaada; Utaratibu wa matibabu ya bure kwa wazee upoje?

Msaada; Utaratibu wa matibabu ya bure kwa wazee upoje?

profesawaaganojipya

JF-Expert Member
Joined
Apr 21, 2015
Posts
1,595
Reaction score
3,416
Ndugu wakuu, nina bibi yangu anaishi Dar na maza, ana umri wa miaka kama 100 hivi, sasa anasumbuliwa sana na maradhi na upande wa uchumi uko vibaya, siwezi mkatia bima ya afya.

Naomba kujua utaratibu wa kupata kitambulisho cha matibabu ya bure kwenye hospitali za Serikali, kwa anaejua...
 
Nenda hospital ya serikali ila uwe na ushahidi wa umri wake. Shida inakuja swala la dawa utanunua. Ila anaweza muona daktari bure kabisa..
 
Nchi yetu kuhusu huduma za afya ni tatizo sana sijui wanataka watu wafe sana labda itasaidia kupunguza idadi ya watu au sijui nini tatizo maana hata suala la bima ya afya kwa wote linapigwa dana dana bila sababu.
 
Nenda hospital ya serikali ila uwe na ushahidi wa umri wake. Shida inakuja swala la dawa utanunua. Ila anaweza muona daktari bure kabisa. .
Bila kitambulisho chochote mkuu? Huo ujasiri ntatoa wapi? Bibi hatembei ntakodi bajaj, halafu nimwambie dkt sina kitu? Sijui kama manesi wa kuandikisha watanielewa.
 
Kata CHF ilioboreshwa kwa 30,000 na itatibu watu 6 kwenye familia ila utaisubiria kwa 2 month kuipata au fika ofisi ya mkurugenzi wa wilaya yako nenda chumba Cha ustawi wa jamii watakusaidia zaidi
 
Kata NHIF ilioboreshwa kwa 30,000 na itatibu watu 6 kwenye familia ila utaisubiria kwa 2 month kuipata au fika ofisi ya mkurugenzi wa wilaya yako nenda chumba Cha ustawi wa jamii watakusaidia zaidi

Hakuna NHIF iliyoboreshwa ya 30000 mkuu,labda kama ulimaanisha iCHF(hii ndo chf iliyoboreshwa na unalipia 30k)
 
Kata CHF ilioboreshwa kwa 30,000 na itatibu watu 6 kwenye familia ila utaisubiria kwa 2 month kuipata au fika ofisi ya mkurugenzi wa wilaya yako nenda chumba Cha ustawi wa jamii watakusaidia zaidi
...Amesema 'Matibabu ya Bure Kwa Wazee
...Hio ya kukata 30,000 Kwa CHF inatoka Wapi Tena?
Ile sera ya ' Matibabu ya Bure Kwa Wazee' iliishia Wapi??
Mbona kama imemezwa na Sera ya 'Bima ya Afya' ?? Au...??'
 
Kata CHF ilioboreshwa kwa 30,000 na itatibu watu 6 kwenye familia ila utaisubiria kwa 2 month kuipata au fika ofisi ya mkurugenzi wa wilaya yako nenda chumba Cha ustawi wa jamii watakusaidia zaidi
CHF ndo nini mkuu,mimi nina bima,nhif,hata mamangu mzazi ana bima ya nhif.
 
Back
Top Bottom