Pole bandubandu,
Kama ulipima malaria kwa BS ikakutwa basi una malaria, endelea kutumia dawa za malaria (japo sijui kwa nini alikupa sindano, ilipaswa utibiwe kwa vidonge, labda kama unikuwa unatapika sana au muoga wa dawa za kumeza). Lakini vile vile ukigundulika na malaria haimaanishi huwezi kuwa/kupata UTI pia, kama ulipima mkojo na ikaonekana una UTI basi pia tumia dawa ulizopewa, Cipro (Ciprofloxacin) ni dawa sahihi na dozi ya kidonge 1*2 ni sahihi.
UTI ni maambukiza ya njia ya mkojo, maambukizi yanaweza panda mpaka level ya mafigo na kusababisha maumivu ya tumbo. Lakini tumbo la chakula na tumbo la uzazi ni matumbo mawili tofauti. Sitegemei maumivu ya tumbo ya UTI yawe sehemu ya chembe. Maumivu ya tumbo sehemu za chembe mara nyingi huwa ni tumbo la chakula, sana sana mfuko wa chakula wenyewe.
Dawa za familia ya NSAIDs (huna haja ya kuijua) ambapo Diclopar ni mojawapo husababisha Gastritis ambayo maumivu ya tumbo kwenye eneo la chembe. Hii ni kwa sababu hizo dawa zikitumiwa kwa wingi/muda mrefu husababisha kudhoofika kwa kuta za mfuko wa tumbo na hivyo acid inayomwagwa kwa kawaida tumboni kuumiza kuta za mfuko wa tumbo.
Ushauri wangu: Endelea na dawa za malaria umalize dozi, Endelea na Cipro umalize dozi, ACHA KUTUMIA DICLOPAR...kama ni muhimu kutumia dawa ya maumivu basi tumia zisozo jamii ya NSAIDs.