Msaada: Utwaaji wa Ardhi

Msaada: Utwaaji wa Ardhi

NANCA

Member
Joined
Jun 23, 2023
Posts
92
Reaction score
100
Je kama hujapewa taarifa ya utwaajwi wa ardhi yako na hata taarifa hiyo ya utwaaji haipo kwenye gazeti la serikali, je hapo Kuna utwaaji? Je utwaaji huo ni halali? Je wapi nikalalamike? Je nani wa kumpelekea malalamiko yangu?

Msaada jamani hasa wenye experience na wanasheria
 
Je kama hujapewa taarifa ya utwaajwi wa ardhi yako na hata taarifa hiyo ya utwaaji haipo kwenye gazeti la serikali, je hapo Kuna utwaaji? Je utwaaji huo ni halali? Je wapi nikalalamike? Je nani wa kumpelekea malalamiko yangu? Msaada jamani hasa wenye experience na wanasheria
Soma Sheria ya Utwaaji wa Ardhi ya Mwaka 1967 pamoja na Marejeo yake yote.
Aidha, pia soma Sheria za Ardhi Na.4 & 5 za Mwaka 1999 pamoja na Marejeo yake yote na Kanuni za Sheria za Ardhi za 2001.
Aidha:-
1.Ardhi hiyo iko wapi hasa?Mjini au Kijijini?
2.Imepimwa au haijapimwa, yaani Surveyed or Unsurveyed Piece of Land??
3.Zoezi au mchakato huo wa Utwaaji wa ardhi umefikia hatua gani?Watu tayari wameshaanza kulipwa fidia yao au bado??

Nijibu kwanza maswali haya ya awali ili nipate mwangaza wa ushauri mzuri wa kukupatia.
 
Kama ulivyoelezwa, kwanza pole kwa kutaka kutawaliwa, hapo hakuna utwaaji ardhi wowote ni wahuni tuu wanataka kupora ardhi yako kwa utapeli wa serikali kutwaa ardhi!.

Utwaaji ardhi wa serikali is a process
1. Kwanza kunaitishwa mkutano wa ushirikishwaji kuwajulisha taarifa ya mabadiliko ya matumizi ya ardhi ya eneo husika linalopangwa kutwaliwa.
2. Mnaelezwa madhumuni ya eneo lenu kutwaliwa, usually is for public utilities, kujenga soko, shule, Hospital, ofisi ya umma au kutenga eneo la uwekezaji.
3. Mnaelezwa msiendeleze chochote, ila kama ni kulima, mlime mazoa ya muda mfupi na sio ya kudumu.
4. Mnafanyiwa tathmini ya kulipwa fidia kwa mazao ya kudumu na kulipwa fidia ya every development mlioifanya kwenye eneo hilo.
5. Tangazo la kutwaa eneo hilo linatangazwa kwenye GN ya serikali.
6. Mkiisha lipwa fidia yenu mnapewa muda wa kuhama na mnaweza kugaiwa eneo jingine kama eneo lilitwaliwa ni la makazi, na miongoni mwa fidia ni kianzio cha kujenga makazi mapya.

Kuna utwaaji ardhi mwingi tuu wa kitapeli, na kuna utwaaji ardhi ambao wananchi mnaombwa mjitolee bure bila kufidiwa kama ni eneo la mapori.

P
 
1.Ardhi ipo wilayani
2.Ardhi haijapimwa
3. Wamefikia hatua ya tadhimini
Binafsi nimegoma kwa kua shijapewa taarifa na hata walokubali ni baada ya kugoma mwanzo wakati wanakuja kusurvey eneo ndo wakaomba kikao kwanza na mtendaji na diwani. Baada ya kukaa na diwani na mtendaji ndio wakakubali wengine wakakataa. Na wengi waliokaa kikao hicho ni wale waliokodi maeneo hayo ili kulima.
Swali langu, je taarifa ya utwaaji inatakiwa kuja wakati gani na katika hatua gani ya utwaaji, je ni kabla hata hawajingia ktk eneo usika au vinginevyo. Na je ktk gazeti la serikali inatangazwa wakati gani? Je wakati mchakato unaendelea au wiki 6 hata kabla rais au wateule wake hawajaingia ktk eneo husika?
* Kiujumla kwa kadri ya uelewa,utaalam wa kisheria na uzoefu je kinachoendelea ni utwaaji au unyang'anyi? Kama ni utwaaji, je ni halali au batili? Msaada maana kabla sijaenda baraza la kata la ardhi au wilaya kujiwekea kinga, lazima niwe na uelewa wa kutosha kutoka kwa wataalam
 
What if Halimashauri wanafika mkwenye eneo na kuweka vigingi na kumgawia mtu bila ushirikishwaji wa aina yoyote?
 
Goma, nenda baraza la ardhi kata, then wilaya Kama hujapata haki, mahakama kuu na mwsho rufaa. Usiwe mnyonge
 
1.Ardhi ipo wilayani
2.Ardhi haijapimwa
3. Wamefikia hatua ya tadhimini
Binafsi nimegoma kwa kua shijapewa taarifa na hata walokubali ni baada ya kugoma mwanzo wakati wanakuja kusurvey eneo ndo wakaomba kikao kwanza na mtendaji na diwani. Baada ya kukaa na diwani na mtendaji ndio wakakubali wengine wakakataa. Na wengi waliokaa kikao hicho ni wale waliokodi maeneo hayo ili kulima.
Swali langu, je taarifa ya utwaaji inatakiwa kuja wakati gani na katika hatua gani ya utwaaji, je ni kabla hata hawajingia ktk eneo usika au vinginevyo. Na je ktk gazeti la serikali inatangazwa wakati gani? Je wakati mchakato unaendelea au wiki 6 hata kabla rais au wateule wake hawajaingia ktk eneo husika?
* Kiujumla kwa kadri ya uelewa,utaalam wa kisheria na uzoefu je kinachoendelea ni utwaaji au unyang'anyi? Kama ni utwaaji, je ni halali au batili? Msaada maana kabla sijaenda baraza la kata la ardhi au wilaya kujiwekea kinga, lazima niwe na uelewa wa kutosha kutoka kwa wataalam
1. Je, mmeambiwa Lengo la huo utwaaji wa ardhi hasa ni nini??Kujenga kiwanda cha mwekezaji?Kujenga majengo/ofisi ya umma?? Mradi wa Upangaji wa Miji (Planning Scheme)??Au nini hasa?
Wadodose kwa undani wahusika ili ujue kwanza kuhusu Jambo hili, ukianzia na ofisi ya Serikali ya Mtaa/Kijiji na ya Afisa Mtendaji wa Kata, ikiwezekana upate documents za matangazo kuhusu suala hili.
2.Je, viongozi gani wa Serikali kutoka Wilayani au Mkoani au Wizarani walikuja ktk mikutano ya uhamasishaji Wananchi kuhusu suala hili?? Je, waliwajulisha kuhusu viwango( rates) za fidia ambayo mnatarajiwa kulipwa??Kwa ekari moja au mita moja ya mraba wanatarajia kulipa fidia kiasi gani??
3.Utaratibu wa Kisheria wa Kupinga Jambo hili ni huu;-
Wananchi ambao hamkubaliani na zoezi hilo mnatakiwa kwa pamoja kwenda kwa Wakili ili awaandalie Hati ya Mashitaka au Hati ya Zuio (Injunction Order) ambayo mtatakiwa kwenda kufungua Kesi Mahakama Kuu ili kumzuia huyo anayetaka kuchukua ardhi yenu bila kufuata utaratibu wa kisheria. Mshitakiwa Namba Moja naamini atakuwa ni Mkurugenzi Mtendaji (DED) wa hiyo Wilaya ulipo na wengineo endapo kama wapo.
NB:- Kesi ya namna hii huwa haifunguliwi ktk Mahakama ya Ardhi ya Kata wala ya Wilaya, zingatia sana suala hili. Kesi husika inatakiwa kufunguliwa ktk Mahakama Kuu tu (Divisheni ya Ardhi).
 
Je kama hujapewa taarifa ya utwaajwi wa ardhi yako na hata taarifa hiyo ya utwaaji haipo kwenye gazeti la serikali, je hapo Kuna utwaaji? Je utwaaji huo ni halali? Je wapi nikalalamike? Je nani wa kumpelekea malalamiko yangu?

Msaada jamani hasa wenye experience na wanasheria
Kama utalipwa, achia hiyo ardhi. Pambana kupata kiasi kikubwa kadri iwezekanavyo.
 
Mleta mada hufunguki vya kutosha ili usaidiwe.

Unaulizwa ardhi ipo wapi, unajibu wilayani; maeneo yote yapo wilayani. Sasa la kwako lipo wilaya ipi?
 
What if Halimashauri wanafika mkwenye eneo na kuweka vigingi na kumgawia mtu bila ushirikishwaji wa aina yoyote?
Lipinge kisheria Jambo hili.
Fanya haya yafuatayo:-
1.Tambua namba za viwanja hivyo vilivyopo kwenye ardhi yako.Pata nakala ya ramani ya upimaji (Survey Map).
2.Andika barua kwa DED kumjulisha kwamba una mpango wa kumshitaki mahakamani (Nottice of Intention to Sue) kwa kitendo chake cha kutwaa ardhi yako bila kufuata utaratibu, kupima viwanja na kisha kuwamilikisha watu wengine bila ya taarifa yoyote kwako.
3.Asipojibu barua yako(ambyo unapaswa kuiandika kwa kupitia kwa Mwanasheria/wakili), basi nenda kafungue kesi Mahakamani.
Mahakama inaweza kuwa ya Wilaya au Mahakama Kuu(Divisheni ya Ardhi) kulingana na thamani ya ardhi husika.
 
Lipinge kisheria Jambo hili.
Fanya haya yafuatayo:-
1.Tambua namba za viwanja hivyo vilivyopo kwenye ardhi yako.Pata nakala ya ramani ya upimaji (Survey Map).
2.Andika barua kwa DED kumjulisha kwamba una mpango wa kumshitaki mahakamani kwa kitendo chake cha kutwaa ardhi yako bila kufuata utaratibu, kupima viwanja na kisha kuwamilikisha watu wengine bila ya taarifa yoyote kwako.

Eneo langu nimegawiwa na kijiji kama shamba
 
Eleza kwa kina scenario ya suala lako, sijakuelewa vizuri.
Mimi na wananchi wenzangu tuilinunua ardhi kwenye serikali ya kijiji kila mtu kwa ukubwa wake, tajiri mmoja akaenda ofisi za ardhi akahonga fedha na kuwaambia eneo hilo analitaka, Mkurugenzi na timu yake akiwemo DC wakawapa vitisho viongozi wa kijiji wakalitwaa eneo na kumpimia huyo tajiri, tulipokwenda kuhoji kulikoni hatushirikishwi tukaambiwa DC na DED wametoa maagizo apimiwe huyo tajiri
 
Mleta mada hufunguki vya kutosha ili usaidiwe.

Unaulizwa ardhi ipo wapi, unajibu wilayani; maeneo yote yapo wilayani. Sasa la kwako lipo wilaya ipi?
Ameuliza ni mjini au kijijini? Pia kwa hatua nliyopo sitakiwi kufungua mambo yote zaidi ya mambo muhim maana kumbuka watwaaji haramu ni wengi na lazima baadhi yao wako humu. Hvyo napshwa kua muangalifu ktk kushughulika nao. Lipo mji unaokua kwa sasa
 
Pambana
 
1.Ardhi hiyo mlinunua (yaani Land Purchase) au Mligawiwa (yaani Land Allocation)???
2.Je, mlipata nyaraka kutoka kwa Ofisi ya Serikali ya Mtaa/Kijiji??
 
Lipinge kisheria Jambo hili.
Fanya haya yafuatayo:-
1.Tambua namba za viwanja hivyo vilivyopo kwenye ardhi yako.Pata nakala ya ramani ya upimaji (Survey Map).
2.Andika barua kwa DED kumjulisha kwamba una mpango wa kumshitaki mahakamani kwa kitendo chake cha kutwaa ardhi yako bila kufuata utaratibu, kupima viwanja na kisha kuwamilikisha watu wengine bila ya taarifa yoyote kwako.
3.Asipojibu barua yako(ambyo unapaswa kuiandika kwa kupitia kwa Mwanasheria/wakili), basi nenda kafungue kesi Mahakamani.
Mahakama inaweza kuwa ya Wilaya au Mahakama Kuu(Divisheni ya Ardhi) kulingana na thamani ya ardhi husika.
Haya madini ndo yakutukwamua wanyonge. Kama jamii forum wangeeka mfumo wa mpesa wa siri basi ngekutumia ya soda kw ushauri huu
 
Back
Top Bottom