Kama ulivyoelezwa, kwanza pole kwa kutaka kutawaliwa, hapo hakuna utwaaji ardhi wowote ni wahuni tuu wanataka kupora ardhi yako kwa utapeli wa serikali kutwaa ardhi!.
Utwaaji ardhi wa serikali is a process
1. Kwanza kunaitishwa mkutano wa ushirikishwaji kuwajulisha taarifa ya mabadiliko ya matumizi ya ardhi ya eneo husika linalopangwa kutwaliwa.
2. Mnaelezwa madhumuni ya eneo lenu kutwaliwa, usually is for public utilities, kujenga soko, shule, Hospital, ofisi ya umma au kutenga eneo la uwekezaji.
3. Mnaelezwa msiendeleze chochote, ila kama ni kulima, mlime mazoa ya muda mfupi na sio ya kudumu.
4. Mnafanyiwa tathmini ya kulipwa fidia kwa mazao ya kudumu na kulipwa fidia ya every development mlioifanya kwenye eneo hilo.
5. Tangazo la kutwaa eneo hilo linatangazwa kwenye GN ya serikali.
6. Mkiisha lipwa fidia yenu mnapewa muda wa kuhama na mnaweza kugaiwa eneo jingine kama eneo lilitwaliwa ni la makazi, na miongoni mwa fidia ni kianzio cha kujenga makazi mapya.
Kuna utwaaji ardhi mwingi tuu wa kitapeli, na kuna utwaaji ardhi ambao wananchi mnaombwa mjitolee bure bila kufidiwa kama ni eneo la mapori.
P