vakolavene
Member
- Jan 20, 2017
- 39
- 26
Habarini wanaforum.
Naombeni msaada nimefuga vifaranga wa kuku wa kienyeji 75 yapata wiki ya pili sasa.Ninawatunza kisasa ndani ya chumba maalumu nikiwapa huduma zote za kuku wa kisasa.
Sasa wiki iliyopita niliona baadhi yao wameanza shusha vibawa vyao. Nikaenda duka la madawa ya kilimo na mifugo, nikaelezwa na muuzaji niwanunulie Esb3 30% yawezekana wana magonjwa ya tumbo. Nilifanya hivyo nikawapa kwa siku tatu kwa kadri nilivyoelezwa, baada ya kumaliza nikaenda kumpa taarifa kua nahisi wanaendelea vizuri, akanishauri pia niwape multivitamin kwa siku tano, nikafanya hivyo na leo naandika thread hii ndio siku ya tano.
Lakini kuna utofauti nimeanza kuuona juzi baada ya kifaranga kimoja kuishiwa nguvu za miguu., ikabidi nikitenge, leo tena alfjiri wakati nawabadilishia moto takribani vifaranga 5 navyo havina nguvu kabisa, nimevurugwa nahisi kama nitawakosa wote. Naombeni msaada nifanye Nn na tatizo litakua Nn?
Tafadhali wanaforum.
Sent using Jamii Forums mobile app