Ushauri wangu Kama ndio unaanza.. Nunua dagaa kutoka kwa wavuvi huko visiwani Kisha nenda kauzie pale Mwaloni Kirumba Mwanza.
Unaweza uza kwa Bei ya Jumla au reja reja.. wanunuzi pale wapo.
My take:- Vijijini hasa huko sijui tabora, Katavi, sumbawanga na nk wahitaji na watuamiji wa hizo dagaa ni wapo na Ni wengi lakini hawana pesa (( Cash in hand hawana )) labda uende ukakopeshe.
Mjini (( Mwaloni Kirumba pale )) wahitaji (wafanya Biashara na watuamiji ) wote wapo na pesa pia wanazo tena cash in hand.. issue bageinini pawa yako katika Bei ya kuuzia.
Back to my Experience.
Nilikuwa naenda kuchukua dagaa tena wale fresh wanene wa jua moja.. kutoka kisiwa Cha GOZIBA.. Nusu nilikuwa nauzia pale Mwaloni Kirumba Mwanza, Mzigo mwingine nilikuwa naupeleka huko Kusini magharibi mwa Tanzania.. Vijiji Kama majimoto, chamalendi, Mamba, inyonga, usevya nk
Faida: Huko Vijijini kote nilikopita zaidi ya kujifunza ukomandoo sikuona faida zaidi ya kuuzia Kirumba Mwanza pale pale. Sababu pale mzunguko unakuwa chapu.